MAGAZETI ya Leo Alhamisi 03 July 2025

MAGAZETI ya Leo Alhamisi 03 July 2025
MAGAZETI ya Leo Alhamisi 03 July 2025

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa, ambaye pia ni Mbunge anayemaliza muda wake wa Jimbo la Ruangwa, ametangaza kutogombea tena nafasi ya ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) hatua iliyoshangaza wengi, hasa baada ya kauli zake za awali kuashiria nia ya kuwania tena nafasi hiyo.
Katika hotuba yake ya kuhitimisha shughuli za Bunge la 12, iliyotolewa Juni 26, 2025, Majaliwa alinukuliwa akisema; “Ninatambua wakati mwingi nimekuwa nje ya jimbo nikilitumikia taifa lakini wana Ruangwa wameendelea kuniunga mkono. Nitumie nafasi hii kusema asanteni sana na ninamuomba Mwenyezi Mungu azidi kuimarisha mshikamano uliopo kati yetu sote. Ninaomba kuwajulisha kuwa ninakuja kuchukua fomu ya kuomba ridhaa yenu tena.”Kauli kama hiyo aliitoa pia katika mkutano wa hadhara uliofanyika Septemba 2024 ambapo alisema, “Wana-Ruangwa wananisikia… nimesema Rais Samia Suluhu Hassan mitano tena na mimi nahitaji tena ubunge… nataka niendelee kuwatumikia, nataka niendelee kuwahudumia.”Hata hivyo Jumatano, Julai 2, 2025, Majaliwa amewashangaza wengi baada ya kutangaza kutogombea tena, alipokuwa akizungumza na wajumbe wa kamati za siasa za Mkoa na Wilaya ya Ruangwa.
Katika hotuba yake ya kuaga, amesema “Imefika wakati kwa mshikamano tulioujenga sasa ni wakati wa kutoa fursa kwa wana-Ruangwa wengine wapenda maendeleo waweze kuunganisha nguvu hizi ili kaulimbiu yetu ya ‘Ruangwa kwa Maendeleo Inawezekana’ iweze kusonga mbele zaidi.”Majaliwa amelihudumia Jimbo la Ruangwa kwa miaka 15 mfululizo, huku akibeba majukumu makubwa ya kitaifa kama Waziri Mkuu wa Tanzania tangu 2015.
JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
