KUITWA Kwenye Usaili Air Tanzania July 2025

KUITWA Kwenye Usaili Air Tanzania July 2025KUITWA Kwenye Usaili Air Tanzania July 2025
Kampuni ya Ndege Tanzania inapenda kuwataarifu wote walioomba kazi katika kada mbalimbali kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 5 Julai, 2025 hadi tarehe 10 Julai, 2025.
Wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
- Usaili utafanyika tarehe 5 Julai, 2025 hadi tarehe 10 Julai, 2025 kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili.
- Muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
- Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi.
- Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkaazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Taifa, Hati ya Kusafiria au Leseni ya udereva.
- Wasailiwa wanatakiwa kufika na vyeti vyao halisi, kuanzia cheti cha Kuzaliwa, Kidato cha IV, VI, Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji.
- Wasailiwa watakaowasilisha “Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”,
hati za matokeo za Kidato cha IV na VI (Form IV and Form VI result slips) HAZITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI. - Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
- Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
- Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo.
- Wasailiwa wenye tofauti ya majina katika vyeti vya elimu, taaluma na cheti cha kuzaliwa wahakikishe wanakuwa na kiapo cha kubadilisha majina kilichosajiliwa (DEED POLL).
- Wasailiwa waliozaliwa nje ya Tanzania wahakikishe wanawasilisha uthibitisho wa uraia kutoka Ofisi za Uhamiaji.
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA MAJINA
Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
