NAFASI Za Kazi Misungwi District Council

Filed in Ajira by on 05.07.2025 0 Comments
Share This Post
NAFASI Za Kazi Misungwi District Council

NAFASI Za Kazi Misungwi District Council

NAFASI Za Kazi Misungwi District Council

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Kumb Na. MZ/MDC/S.10/25/102 04/07/2025

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wialaya ya Misungwi amepata kibali kipya cha ajira kwa ikama ya mwaka 2024/2025 chenye Kumb.Na FA.97/228/01/A/25 cha tarehe 29 Aprili 2025 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Kufuatia kibali hicho Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Misungwi anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye Sifa za Kujaza nafasi za Kazi Mbalimbali zilizoanishwa hapa chini.

✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – NAFASI NNE (04)

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kuorodhesha barua zinazoingia masijala mwenye regista (Incoming
    Correspondence Register).
  • Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi (Outgoing
    CorrespondenceRegister).
  • Kusambaza majalada kwa watendaji (Action Officers).
  • Kupokea majalada yanayorudi masijala kutoka kwa watendaji.
  • Kurudisha majalada kwenye shubaka/kabati la majalada (Racks/FillingCabinets) au Mahali Pengine yanapohifadhiwa.
  • Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani na nje ya Taasisi (File tracking).

SIFA ZA MWOMBAJI.
Awe na Elimu ya kidato cha Nne (IV) au cha Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya
stashahada/Diploma (NTA Level 6) katika fani ya utunzaji wa kumbukumbu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, mwenye ujuzi wa Kompyuta.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS C

✅DEREVA DARAJA LA II NAFASI NANE (08)

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
  • Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
  • Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
  • Kutunza na kuandika daftari la safari “log book” kwa safari zote.
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
  • Kufanya usafi wa Gari.
  • Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
  • Kuajiriwa wenye cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo wamefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika.
  • Wawe wamehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au Chuo kingine
    kinachotambuliwa na Serikali

MAELEKEZO YA JUMLA.

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na usiozidi miaka 45.
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira Ulemavu walionao kwaajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya ajira katika Utumishi wa Umma.
  • Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na anuani ya barua pepe (E- mail Address) pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa
    kuaminika.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika
    Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificate – Cheti cha Mtihani wa Kidato cha nne na cha Sita, Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Proffessional Certificate from Respective Boards).
  • Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips)
    HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTVET).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi wa kada ya Dereva II wenye leseni Daraja E au C wanapaswa KUAMBATISHA vyeti vya mafunzo ya Udereva vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba,
    2010.
  • Waombaji watakaowasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.
  • Wasailiwa ambao majina yao yanatofautiana katika nyaraka zao wanapaswa kuwasilisha Hati ya Kiapo cha Kubadili Jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi.

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya Elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi,
S.L.P 20,
MISUNGWI.

Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa ajira
(Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz (Anuani
hii pia inapatikana kwenye Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu
iliyoandikwa “Recruitment Portal”

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo
hili HAYATAFIKILIWA.

Mwisho wa Kutuma Maombi ni tarehe 17 Julai 2025

JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?
Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, GROUP NO 2 HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA, GROUP NO 3 HAPA, GROUP NO 4 HAPA


Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *