71 Wafutiwa Matokeo Kidato Cha Sita 2025

Filed in Elimu by on 07.07.2025 0 Comments
Share This Post
71 Wafutiwa Matokeo Kidato Cha Sita 2025

71 Wafutiwa Matokeo Kidato Cha Sita 2025

71 Wafutiwa Matokeo Kidato Cha Sita 2025

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Baraza la Mitihani la Tanzania limefuta matokeo ya watahiniwa 71, wakiwemo 70 wa mtihani wa kidato cha sita na mmoja wa ualimu daraja A (GATCE).

Akitangaza matokeo hayo leo Julai 7, 2025 katika ofisi za baraza hilo Zanzibar, Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Profesa Said Mohamed amesema kuwa matokeo hayo yamefutwa kwa mujibu wa kifungu cha 5(2) (i) na (j) cha shera ya baraza la mtihani sura ya 107.

“Kifungu hiki kinasomwa pamoja na kifungu cha 30 (2) (b) cha kanuni za mitihani za mwaka 2016,” amesema.

Kwa mujibu wa Profesa Mohamed, baadhi yao waliingia na simu, saa janja kwenye vyumba vya mtihani na kusaidiana kwenye mtihani.

“Ni udanganyifu umefanywa na watahiniwa wenyewe, baadhi yao wamesaidiana kwenye chumba cha mtihani, kuna walioingia na simu, smart watch, baadhi yao wameingia na karatasi zenye majibu kinyume cha sheria,” amesema.

Ameongeza kuwa: “Baadhi yao tumewakuta katika karatasi za kujibia wana miandiko inayofanana na kuona mfanano ambao sio wa kawaida, hivyo huo nao ni udanganyifu kinyume cha sheria.”

JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?
Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, GROUP NO 2 HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA, GROUP NO 3 HAPA, GROUP NO 4 HAPA


Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *