NAFASI Za Kazi Mtama District Council

NAFASI Za Kazi Mtama District Council
NAFASI Za Kazi Mtama District Council
Kumb. Na. MDC/I.9/1/VOL.III/51 09/07/2025
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama amepokea kibali cha Ajira mpya kwa ikama ya mwaka 2024/2025 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora chenye Kumb. Na. FA.97/288/01/A/25 cha tarehe 29/04/2024.
Hivyo Watanzania wote wenye sifa wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kwa nafasi zifuatazo:-
✅DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 2
MAJUKUMU YA KAZI YA DERAVA DARAJA LA II
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
- Kupeleka Watumishi kwenye Safari za Kazi.
- Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari.
- Kukusanya na kusambaza Nyaraka mbalimbali pale inapohitajika.
- Kujaza na kutunza taarifa za Safari zote katika daftari la Safari.
- Kufanya Usafi wa gari.
- Kazi nyingine anazopangiwa na mwajiri.
SIFA ZA KUAJIRIWA
Mwombaji awe mwenye elimu ya kidato cha Nne (Form IV) au Sita (Form VI) na Leseni ya Daraja C au E ya Uendeshaji Magari ambayo wamefanyia kazi kwa muda usiopungua wa mwaka mmoja
(1) bila kusababisha ajali pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika. Wawe wamehudhuria mafunzo ya Misingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course)
yanayotolewa na Chuo cha VETA au Chuo kingine kinachotambulika na Serikali.
MSHAHARA: Kwakuzingatia ngazi za Mishahara ya Serikali TGS B.
✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI 1
MAJUKUMU YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II
- Kuorodhesha barua zinazoingia Masjala kwenye regista (incoming
correspondence register). - Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi (outgoin correspondence register).
- Kusambaza majalada kwa Watendaji (Action Officers).
- Kupokea majalada kwa Watendaji (Action Officers).
- Kupokea majalada yanayorudi masjala toka kwa Watendaji.
- Kurudisha majalada kwenye Shabaka/ Kabati la Majalada (racks/Filling cabinets)
au mahali pengine yanapohifashiwa na - Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi (File tracking)
SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji awe na Cheti cha Kidato cha Nne (IV) AU Kidato cha Sita (VI) aliyehitimu Stashahada (NTA Level 6) katika fani ya Masijala kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, mwenye ujuzi wa Kompyuta
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za Mishahara ya Serikali TGS C.
MASHARTI YA JUMLA.
- Waombaji wote wawe raia wa Tanzania na wenye umri kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwaajili ya taarifa
kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishiwa wa Umma. - Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detail Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua pepe (E- mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika;
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/ Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia
kiwango hicho na Vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi
husika. Postgraduate/ Degree/Advanced Diploma/Certificate – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Proffessional
Certificate from Respective Boards) - Wasailiwa watakaowasilisha “Testmonial” Provisioinal Result” “Statement of result” hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA na HAWATATUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
- Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vinahakikiwa na vimethibitishea
na Mamlaka husika (TCU, NECTA NA NACTE). - Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwei kuomba isipokuwa kama wanakibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kingozi.
- Waombaji kazi wa wa kada ya Dereva II wenye leseni Daraja E au C wanapaswa KUAMBATISHA vyeti vya mafunzo ya Udereva vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika.
- Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
- Waombaji kazi watakaowasilisha taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za Kisheria.
- Wasailiwa ambao majina yao yanatofautiana katika nyaraka zao wanapaswa kuwasilisha Hati ya Kiapo cha kubadili jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi.
MUHIMU: Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja
nav yeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-
Mkurugenzi Mtendaji Wa Halmashauri
Halmashauri Ya Wilaya Ya Mtama
S.L.P 328,
MTAMA
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa Kielektroniki wa Ajira (Recrutment portal) kupitia anuani ifuatayo: https://portal.ajira.go.tz. Anuani hii inapatikana pia kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recrtutment portal’
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioanishwa katika tangazo hili
HAYATAFIKIRIWA.
Mwisho wa Kutuma Maombi ni tarehe 23/07/2025.
| POST: MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – 1 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Mtama More Details |
2025-07-23 Login to Apply |
| POST: DEREVA DARAJA II – 2 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Mtama More Details |
2025-07-23 Login to Apply |
Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.

YAH.MAOMBI YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU
Rejea kichwa cha habari hapo juu.
Ninayo heshima kubwa kutuma maombi yangu ya msaidizi wa kumbukumbu katika halmashauri ya wilaya ya mtama .Elimu yangu ni kidato cha 4 na nimesoma katika chuo cha utumishi wa umma ngazi ya cheti na diploma.Namba yangu ni 0782542272
Nitashukuru sana iwapo ombi langu litakubaliwa
Wako mtiifu
Naomi Gideon