NAFASI Za Kazi Chunya District Council

NAFASI Za Kazi Chunya District Council
NAFASI Za Kazi Chunya District Council
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya amepokea kibali cha Ajira Mpya kwa Ikama ya mwaka wa fedha 2024/2025 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chenye Kumb. Namba FA.97/288/01/A/25 ya tarehe 29/04/2025.
Hivyo Watanzania wote wenye sifa wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kwa nafasi zifuatazo:-
✅DEREVA II – NAFASI 5
KAZI NA MAJUKUMU
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
- Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kazi.
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
- Kutunza na kuandika daftari la safari “ log book’’ kwa safari zote.
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
- Kufanya usafi wa gari na
- Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
SIFA ZA MWOMBAJI:
Kuajiriwa wenye cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au c ya uendeshaji magari ambayo wamefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali pamoja nav yeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika. Wawe wamehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic
Driving Course) yanatolewa na Chuo cha VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na
Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingazia Ngazi ya Mishahara ya Serikali TGS B
✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI II – NAFASI 2
KAZI NA MAJUKUMU.
- Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri.
- Kupokea wageni na kuwasikiliza shida zao, na kuwaelekeza sehemu
wanapoweza kusaidiwa. - Kutunza taarifa na kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine.
- Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi.
- Kupokea majalada na kusambaza kwa maofisa walio katika Idara/Kitengo/ Sehemu husika.
- Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika.
- Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali na
- Kuandaa orodha ya mahitaji ya ofisi.
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajirirwa mhitimu wa kidato cha nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) wenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA level 6 ya uhazili kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali. Aidha, awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na Awe amepata mafunzo ya programu za kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, Powerpoint, Internet, Email na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingazia Ngazi ya Mishahara ya Serikali TGS C
✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II- NAFASI 2
KAZI NA MAJUKUMU
- Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye rejista (incoming correspondence register).
- Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasisi kwenye rejista (outgoing
correspondence register). - Kusambaza majalada kwa watendaji (Action Officers).
- Kupokea majalada yanayorudi masjala toka kwa watendaji (Action Officers).
- Kutafuta kumbukumbu/ nyaraka/majalada yanayohitajika na watendaji (Action Officers).
- Kurudisha majalada kwenye shubaka/kabati la majalada (ranks/filling cabinets) au
mahali pengine yanapohifadhiwa. - Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya taasisi ( File tracking);
SIFA ZA MWOMBAJI:
Mwombaji awe na cheti cha Kidato cha Nne (IV) au kidato cha Sita (VI) aliyehitimu Stashahada (NTA level 6) katika fani ya Masijala kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, mwenye ujuzi wa Kompyuta.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingazia Ngazi ya Mishahara ya Serikali TGS C
MASHARTI YA JUMLA KWA MUOMBAJI
- Waombaji wote wawe raia wa Tanzania na wenye umri kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwaajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
- Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detail Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya
Barua pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika. - Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/ Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na Vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Proffessional Certificate from Respective Boards)
v. Wasailiwa watakaowasilisha “Testmonial” “Provisioinal Result”,”Statement of result”, hati za matokeo ya Kidato cha IV na VI (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA
NA USAILI - Wapombaji waliosoma nje Nchi wahakikishe vyeti vyao vinahakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA NA NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji kazi wa kada ta Dereva II wenye leseni Daraja E au C wanapaswa KUAMBATISHA vyeti vya mafunzo ya Udereva vilivyowapatia sifa ya kupata
madaraja husika. - Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
- Waombaji watakaowasilisha taarifa na sifa za kugushi watachukuliwa hatua za kisheria.
- Wasailiwa ambao majina yao yanatofautiana katika nyaraka zao wanapaswa kuwasilisha Hati ya Kiapo cha kubadili jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi.
MUHIMU: Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-
Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri Ya Wilaya Ya Chunya,
S. L. P 73
CHUNYA
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anauani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ . Anuani hii inapatikana pia kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’.
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIKIWA.
Mwisho wa Kutuma Maombi ya Kazi ni tarehe 23/07/2025
| POST: MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – 2 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Chunya More Details |
2025-07-23 Login to Apply |
| POST: MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – 2 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Chunya More Details |
2025-07-23 Login to Apply |
| POST: DEREVA DARAJA II – 5 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Chunya More Details |
2025-07-23 Login to Apply |
Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
