NAFASI Za Ufadhili Wa Masomo Samia Scholarship Extended Data Science/Artificial Intelligence 2025/2026

NAFASI Za Ufadhili Wa Masomo Samia Scholarship Extended Data Science/Artificial Intelligence 2025/2026
NAFASI Za Ufadhili Wa Masomo Samia Scholarship Extended Data Science/Artificial Intelligence 2025/2026
NAFASI Za Ufadhili Wa Masomo Katika Vyuo Vikuu Bora Duniani Katika Fani Za Sayansi Ya Data, Akili Unde Na Sayansi Shirikishi Kwa Mwaka 2025/2026 (Samia Scholarship Extended Data Science/ Artificial Intelligence +)
UTANGULIZI
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatangaza fursa za ufadhili wa masomo katika ngazi ya Shahada ya Kwanza na Shahada ya Umahiri kupitia programu ya SAMIA SCHOLARSHIP EXTENDED DS/AI+ (SSE- DS/AI+) kwa mwaka wa masomo 2025/26.
Programu ya SAMIA SCHOLARSHIP EXTENDED DS/AI+ itatoa ufadhili kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao ya awali na wanaotaka kujiendeleza kitaaluma katika fani za “Data Science, Artificial Intelligence, Cybersecurity, Machine learning na Allied Sciences”.
Ufadhili huu ni wa asilimia mia moja (100%) ukijumuisha ada ya masomo, udahili wa chuo na usajili wa kozi, gharama za utafiti, posho ya kujikimu, bima ya afya, usafiri, makazi na gharama za kujifunza lugha.
UFADHILI WA SHAHADA YA KWANZA
- Ufadhili huu utatolewa kwa wahitimu wa kidato cha sita ambao majina yao yameorodheshwa kwenye Tovuti rasmi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (https://www.moe.go.tz)
Mwombaji wa ufadhili awe na sifa zifuatazo:
- Awe Mtanzania.
- Awe na ufaulu wa juu kwenye mitihani ya Taifa ya kidato cha sita mwaka 2025 iliyoendeshwa na NECTA katika tahasusi za PCM, PGM au PMC; na ambaye jina lake limeorodheshwa kwenye tovuti rasmi za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, COSTECH, au NM-AIST.
Mafunzo ya shahada ya kwanza yatatanguliwa na kambi ya mafunzo ya maandalizi (Bootcamp) ambayo yatafanyika katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, iliyopo Tengeru-Arusha kwa kipindi cha miezi kumi (10).
Ufadhili wa SAMIA SCHOLARSHIP EXTENDED DS/Al+ ni wa muda wa miaka mitatu (03) hadi mitano (05) kulingana na programu husika walizodahiliwa.
Maombi ya SSE- DS/AI+ kwa shahada ya kwanza yatafanyika kwa mwanafunzi na mzazi/mlezi kujaza fomu maalumu iliyoambatishwa, na kuwasilisha kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa njia ya barua pepe ps@moe.go.tz.
(Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 8 Agosti, 2025.)
UFADHILI WA SHAHADA YA UMAHIRI
Ufadhili huu utatolewa kwa wanafunzi waliohitimu shahada ya kwanza wenye sifa zifuatazo:
- Awe Mtanzania.
- Awe na udahili wa kusoma shahada ya Umahiri katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) au IIT Madras Zanzibar kozi za Data Science, Artificial Intelligence, Cybersecurity Machine Learning na Allied Sciences.
- Awe na umri usiozidi miaka 35.
Awe na GPA isiyopungua 3.8 katika shahada ya kwanza/ Kiwango kingine kinachotambulika na Chuo husika. - Wanafunzi wanufaika, watagharamiwa kwa kipindi kisichozidi miaka miwili ya
masomo.
Ufadhili wa masomo ya umahiri kupitia SSE-DS/AI+ utajumuisha yafuatayo;
- Ada ya masomo.
- Posho ya kujikimu.
- Bima ya afya.
- Gharama za Utafiti kwa mujibu wa miongozo ya Chuo.
- Gharama za udahili na
- Usajili wa kozi.
Maombi ya Ufadhili kwaajili ya shahada ya Umahiri yawasilishwe kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa njia ya barua pepe ps@moe.go.tz kuanzia tarehe 1 Oktoba hadi 30 Oktoba, 2025.
MASHARTI YA UFADHILI
Mwanafunzi atakayepata ufadhili wa SAMIA SCHOLARSHIP EXTENDED DS/AI+ atatakiwa kuzingatia masharti yafuatayo:
- Anapaswa kusoma, kuelewa na kusaini Mkataba wa Makubaliano ya Ufadhili wa Masomo kati yake na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
- Anapaswa kuwa na akaunti ya Benki kwa ajili ya kuwezesha malipo ya fedha za ufadhili.
- Mnufaika hataruhusiwa kubadilisha programu ya masomo aliyopatia ufadhili bila idhini ya maandishi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
- Wanufaika watatakiwa kuwa na ufaulu wa 3.8 kwa kila mwaka au kiwango kingine cha ubora wa juu kinachotambuliwa na chuo husika.
- Mnufaika hataruhusiwa kuahirisha masomo, isipokuwa kwa sababu za kiafya, au kijamii zilizothibitishwa.
Ikiwa mnufaika ataahirisha fursa ya ufadhili kabla ya kuanza masomo, atapaswa kuwasilisha taarifa ya maandishi kwa:
Katibu Mkuu,
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,
Mji wa Serikali Eneo la Mtumba Mtaa wa Afya, S.L.P 10,
40479 DODOMA, TANZANIA.
Barua pepe: ps@moe.go.tz
Imetolewa na:
Katibu Mkuu,
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
Julai 9, 2025
DODOMA
Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
