NAFASI Za Ufadhili wa Masomo Kwa Wanachuo wa Stashahada ya Ualimu Elimu Maalumu 2025/2026

Filed in Elimu by on 20.08.2025 0 Comments
Share This Post
NAFASI Za Ufadhili wa Masomo Kwa Wanachuo wa Stashahada ya Ualimu Elimu Maalumu 2025/2026

NAFASI Za Ufadhili wa Masomo Kwa Wanachuo wa Stashahada ya Ualimu Elimu Maalumu 2025/2026

NAFASI Za Ufadhili wa Masomo Kwa Wanachuo wa Stashahada ya Ualimu Elimu Maalumu 2025/2026

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU FURSA YA UFADHILI WA MASOMO KWA WANACHUO WA STASHAHADA YA UALIMU ELIMU MAALUMU
KWA MWAKA WA MASOMO 2025/2026

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatangaza fursa ya Ufadhili wa Masomo ngazi ya Stashahada ya Ualimu wa Elimu Maalumu.

Maombi yanakaribishwa kwa wanachuo wanaosoma, Stashahada ya Elimu maalumu katika maeneo yafuatayo:

  • Ulemavu wa Akili.
  • Usonji.
  • Uziwi.
  • Uziwi Kutoona na
  • Ulemavu wa Uoni.

SIFA ZA KUPATA UFADHILI
Ufadhili huu utatolewa kwa wanafunzi wenye sifa zifuatazo:

  • Awe Mtanzania.
  • Awe amepata udahili katika Chuo cha Ualimu kinachotambulika na Serikali na kinatoa Stashahada ya Ualimu Elimu Maalumu;

NAKALA ZA KUWASILISHA

  • Barua ya kuomba ufadhili ikionesha kozi unayosoma, namba ya simu na barua pepe.
  • Nakala ya vyeti vya kitaaluma vilivyothibitishwa na mwanasheria.
  • Cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na mwanasheria na
  • Barua kutoka kwa Mkuu wa Chuo ikionesha kuwa umedahiliwa katika Chuo husika.

MAENEO YA UFADHILI
Ufadhili utahusisha maeneo yafuatayo:

  • Ada ya Mafunzo.
  • Michango mingine ya Chuo (Mf. Ulinzi, ukarabati n.k).
  • Vifaa vya kufundishia na kujifunzia.
  • Nauli na
  • Bima ya Afya.

MASHARTI YA UFADHILI
Mwanachuo atakayepata ufadhili kwa ajili ya kusoma Stashahada ya Elimu Maalumu atawajibika kuzingatia masharti yafuatayo:

  • Anapaswa kusoma, kuelewa na kusaini Mkataba wa Makubaliano ya Ufadhili wa Masomo kati yake na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
  • Anapaswa kuwa na akaunti ya Benki kwa ajili ya fedha atakazolipwa moja kwa moja.
  • Mnufaika hataruhusiwa kubadilisha programu ya masomo aliyopatia ufadhili bila idhini ya Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
  • Mnufaika hataruhusiwa kuahirisha masomo, isipokuwa kwa sababu za kiafya, na kuthibitishwa na Daktari kutoka katika Kituo cha Afya au Hospitali inayotambuklika na Serikali.
  • Ikiwa mnufaika ataghairi fursa ya ufadhili, atapaswa kutoa taarifa kwa maandishi kwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia kwa Mkuu wa chuo alichodahiliwa na kujisajili.

MUDA WA UFADHILI
Ufadhili huu ni kwa kipindi cha miaka miwili (02) ya masomo kwa wanachuo watakaokidhi vigezo viliyobainishwa katika kipengele Na. 5.

UTARATIBU WA KUOMBA UFADHILI
Maombi yawasilishwe Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ndani ya siku 15 kuanzia Agosti 18 hadi 28, 2025.

Maombi yatumwe kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, S.L.P 10 Dodoma.

Orodha ya Wanachuo watakaokuwa wamepata ufadhili huo itawekwa katika tovuti ya Wizara (www.moe.go.tz).

JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?
Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, GROUP NO 2 HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA, GROUP NO 3 HAPA, GROUP NO 4 HAPA


Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *