MAGAZETI ya Leo Jumapili 24 August 2025

MAGAZETI ya Leo Jumapili 24 August 2025
MAGAZETI ya Leo Jumapili 24 August 2025

Wanandoa wanaodaiwa kuwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wameuawa katika Kijiji cha Chafuma, wilayani Momba.
Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na Jeshi la Polisi Agosti 23, 2025 tukio la mauaji lilitokea Kata ya Kapele iliyo Tarafa ya Ndalambo, juzi Agosti 22, saa nane mchana.
Taarifa hiyo iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Augustino Senga imesema kuwa wanandoa hao waliuawa kikatili kwa kupigwa na kuchomwa moto na wananchi waliojichukulia sheria mkononi wakiwatuhumu kuhusika na mauaji ya Imbanji Simwaka (80), aliyekuwa mama mwenye nyumba waliyokuwa wakiishi.
Amewataja waliouawa kuwa ni Babuloha mwenye umri kati ya miaka 26 na 28, pamoja na Jenifa Babuloha anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 23 na 25, ambao inaelezwa waliingia nchini kinyemela bila kufuata utaratibu wa kisheria.
Kamanda Senga amesema Simwaka aliuawa usiku wa Agosti 19, 2025 kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani.
Amesema mwili wake ulifukiwa bafuni nyumbani kwake na tangu Agosti 20, hakuonekana hali iliyozua wasiwasi miongoni mwa ndugu na wanakijiji.
JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
