NAFASI 40 Za Kazi Bahi District Council

NAFASI 40 Za Kazi Bahi District Council
NAFASI 40 Za Kazi Bahi District Council
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi anatangaza nafasi Arobaini(40) za kazi ya Mkataba ya wakusanyaji mapato (revenue collectors) ambao wataajiriwa kwa muda wa miezi minne (4) kuanzia tarehe 1 Septemba, hadi Tarehe 30, Disemba 2025 kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Mapato hayo yatakusanywa katika vyanzo mbalimbali vya mapato kama vitakavyoonekana kwenye Mikataba itakayoandaliwa baada ya taratibu za ajira ya muda kukamilika.
MAJUKUMU YA KAZI.
- Kukusanya mapato kutoka kwenye vyanzo vya mapato atakavyopangiwa.
- Kuhakikisha kuwa makusanyo yote yaliyokusanywa kwa siku hiyo yanawekwa Benki.
- Kuhakikisha kuwa makusanyo yote yanakusanywa kwa kutumia mashine ya kukusanyia mapato (POS MACHINE) na kutoa stakabadhi halali za Halmashauri.
- Kuhakikisha kuwa mashine ya kukusanyia mapato (POS MACHINE) inakuwa katika hali ya usalama na inatumika muda wote bila kuzimwa (inakuwa ONLINE).
- Kuhakikisha kuwa mteja anapata risiti yake ya ushuru/tozo aliolipia kwa wakati pasipo kuchukua pesa mkononi bila kutoa risiti.
- Kufanya kazi yoyote inayohusiana na ukusanyaji na usimamizi wa mapato utakayopangiwa na msimamizi wa kazi na mahali popote katika Halmashauri ya Wilaya ya Bahi.
Malipo kwa kazi hii ni asilimia 10% ya makusanyo yatakayokusanywa na kuwekwa benki na mkusanya mapato katika chanzo husika kwa kila mwezi.
SIFA MUHIMU ZA WAOMBAJI:
- Awe raia wa Tanzania ambaye ni mkazi wa Halmashauri ya Bahi.
- Awe na kitambulisho cha Taifa (NIDA).
- Awe amehitimu kidato cha nne na kuendelea.
- Awe na ujuzi wa kutumia kwa ufasaha simu janja (smart phone) au Pos.
- Mwombaji anatakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye mali zisizohamishika katika maeneo wanayotoka na aliye tayari kuchukuliwa mali zake bila masharti yeyote mwombaji akiajiriwa endapo atapatikana na upotevu wa pesa za mwajiri.
- Mwombaji anatakiwa kuambatanisha picha mbili (passport size) za rangi za hivi karibuni.
- Mwombaji atakayekidhi sifa zinazotakiwa ataajiriwa na kupangwa kukusanya mapato katika vyanzo mbalimbali vya mapato vya Halmashauri ya Bahi.
MASHARTI KWA WAOMBAJI WA AJIRA HII:
- Awe na Kitambulisho cha Taifa(NIDA).
- Awe na umri wa miaka 18 hadi 45.
- Awe anajua kusoma na kuandika kwa ufasaha lugha ya kingereza au Kiswahili.
- Awe mwaminifu, mwadilifu, na mwenye weledi.
- Awe hajawai kupatikana na hatia kwa makosa ya jinai.
- Mwombaji asiwe na deni lolote Halmashauri ya Bahi katika mifumo yote miwili (TAUSI na LGRCIS) kwa wakusanya mapato waliowai kufanya kazi na Halmashauri ya Bahi
- Barua ya maombi ipitie kwa Mtendaji wa Kijiji.
- Barua ya Maombi iwe na namba za simu na anwani ya kuaminika.
- Majina kamili ya wadhamini na namba zao za simu zinazopatikana.
Barua za maombi ziandikwe kwa mkono zikiwa na viambatanisho vinavyohitajika kama vile vivuli vya vyeti vyake vya elimu, NIDA na zitumwe kwa Anwani.
MKURUGENZI MTENDAJI
HALMASHAURI YA BAHI, S.L.P 2993
DODOMA.
Maombi yanapokelewa kuanzia tarehe 22/08/2025 hadi 01/09/2025 saa 9:00 Alasiri, katika ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya BAHI.
JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
