NAFASI Za Kazi Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Singida

Filed in Ajira by on 25.08.2025 3 Comments
Share This Post
NAFASI Za Kazi Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Singida

NAFASI Za Kazi Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Singida

NAFASI Za Kazi Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Singida

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Singida anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi za kujitolea katika kada ya Udereva na Utunzaji kumbukumbu (Mapokezi).

✅DEREVA DARAJA LA II-NAFASI 2
1.1 Majukumu ya kazi ya Dereva Daraja la II

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
  • Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
  • Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari.
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
  • Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari.
  • Kufanya usafi wa gari.
  • Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na msimamizi wake wa kazi.

SIFA ZA MWOMBAJI

  • Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na chuo cha VETA au NIT au chuo kingine kinachotambuliwa na serikali.
  • Awe na leseni ya udereva daraja C au E.
  • Awe na cheti cha ufaulu wa mtihani wa kidato cha IV.
  • Mwombaji mwenye cheti cha majaribio ya ufundi atafikiriwa kwanza.
  • Awe na umri usiopungua miaka 18  na usiozidi miaka 45.
  • Mwenye uzoefu wa kazi atapewa kipaumbele.

✅MAPOKEZI(RECEPTIONIST)-NAFASI 4

MAJUKUMU YAKE:

  • Kupokea wateja na kuingiza taarifa kwenye mfumo kwa ajili ya kuonana na daktari.
  • Kuelekeza wateja mahali pa kupatiwa matibabu.
  • Kutunza kumbukubu za wateja kupitia mfumo wa matibabu.
  • Kutoa maelekezo sahihi kwa wateja juu ya taratibu za kulipia matibabu na kuingiza kwenye mfumo.
  • Kutunza fomu za Bima ya afya na kuziwasilisha kwa wakati Kitengo cha bima.
  • Kutunza kumbukumbu za wagonjwa na kuhakikisha zinapatikana kwa wakati zinapohitajika.
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu uzoefu na ujuzi wake.

SIFA ZA MWOMBAJI

  • Waombaji lazima wawe wahitimu wenye Astashahada katika fani ya Utunzaji wa Kumbukumbu kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
  • Awe na Elimu ya kidato cha nne.
    Awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45.
  • Awe raia wa Tanzania na ambaye hajawai kushtakiwa kwa makosa ya jinai.
  • Mwenye uzoefu wa kazi na uwezo wa kutumia kompyuta atapewa kipaumbele.

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

  • Mwombaji awe Raia wa Tanzania na mwenye umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45.
  • Kila mwombaji anatakiwa aambatishe nakala ya vyeti vya Elimu ya Sekondari na taalumavinavyohitajika kulingana na Kada husika kama ilivyofafanuliwa katika tangazo hili.
  • Kila Mwombaji aambatishe nakala ya cheti cha kuzaliwa.
  • Uwasilishaji wa vyeti vya kugushi utapelekea kuchukuliwa hatua za kisheria.
  • Mwombaji aambatanishe Wasifu binafsi (CV) akionesha uzoefu, namba za simu, anuani yake na anuani za wadhamini watatu (3) wa uhakika.
  • Mwombaji aambatishe picha ndogo (Passport size) mbili (2) kwenye barua ya maombi.
  • Mwombaji aambatanishe nakala ya Kitambulisho cha NIDA au namba ya NIDA.
  • Waombaji watakaokidhi vigezo wataitwa kwenye usaili na watakaoshindwa kuzingatia masharti ya Tangazo hili hawataitwa.

Aidha atakaewasilisha barua yake kwa njia ya mkono ahakikishe anasaini kitabu maalumu cha kupokea barua hizi masijala.

Maombi yanaweza kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili au Kingereza
Maombi yote yatumwe au yawasilishwe ofisi ya Masjala ya wazi au kupitia barua pepe; barua@sigidarrh.go.tz kwa anuani ifuatayo:-
Mganga Mfawidhi,
Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Singida,
S.L.P 104,
SINGIDA.

Mwisho wa Kupokea Barua za Maombi ni tarehe 30.08.2025 saa 9:30 Alasiri.

JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?
Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, GROUP NO 2 HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA, GROUP NO 3 HAPA, GROUP NO 4 HAPA


Share This Post

Tags:

Comments (3)

Trackback URL | Comments RSS Feed

  1. Hello Dear Sir/madam
    My name is Shabani Itemwa shinura I’m very interested to request for this job to join in order to contribute the organization performance development in order to afford the economy development process.

  2. Enock Kawogo says:

    Thanks for this oppotunity which you give to as, and will be in the first line to take this oppotunity as a part of implementing and applying our knowlegy into a realy practical and gain more experience in record managment

  3. Enock Kawogo says:

    Samahani nimejaribu kutuma ombilangu mara tatu lakini email haijafanikiwa ku submit ombi langu sijajua nimekosea wapi au shida nini, naomba msaada kama itawezekana.

    ninapata ujumbe huu pindi niki submit ombi langu

    ” Delivery has failed to these recipients or groups:

    barua@sigidarrh.go.tz
    The recipient’s email address isn’t correct. Please check the email address and try to resend the message. If the problem continues, contact your email admin. ”

    Naomba msaada tafathari, i real need this oppotunity 🥲🥲🥲🥲🥲🥲🥲

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *