MAGAZETI ya Leo Jumatano 27 August 2025

MAGAZETI ya Leo Jumatano 27 August 2025
MAGAZETI ya Leo Jumatano 27 August 2025
Chama cha ACT Wazalendo kimesema kuwa kimepokea taarifa kutoka kwa Msajili wa Vyama vya Siasa juu ya uamuzi wake wa kutengua ugombea wa Luhaga Joelson Mpina kuwa Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya ACT Wazalendo ambapo ACT imesema itafungua kesi Mahakama Kuu kupinga hatua hii ya Msajili wa Vyama vya Siasa na katika kesi hiyo, ACT itaweka zuio (injunction) dhidi ya utekelezwaji wa uamuzi huu hadi kesi ya msingi isikilizwe.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa ACT, Ado Shaibu imesema “Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Chama inaipitia kwa umakini hatua hii ya Msajili wa Vyama vya Siasa na katika wakati muafaka tutatoa mwelekeo wetu wa kina”
“Wakati uchambuzi wa awali ukiendelea kufanyika tunapenda kutoa msimamo wetu wa awali juu ya suala hili kama ifuatavyo, ACT Wazalendo inaweka msimamo kuwa hakitofuata maelekezo ya Msajili wa Vyama vya Siasa juu ya suala hili kwa sababu katika mazingira ambayo mchakato wa uchaguzi umeshaanza, Tume ya Uchaguzi imeshatoa fomu na wagombea wakiendelea na taratibu za ujazaji na urejeshaji wa fomu, Msajili wa Vyama vya Siasa hana mamlaka ya kuingilia mchakato huo isipokuwa kwa njia ya pingamizi”
“Mgombea wetu wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Luhaga Joelson Mpina amechukua fomu, amezijaza, amezunguka nchi nzima kusaka wadhamini, amekula kiapo mahakamani na kukamilisha taratibu zote zinazohusu ukamilishaji wa fomu za kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”
“Leo tarehe 26 Agosti 2025 fomu hizo zimehakikiwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na kesho saa 7.00 mchana zitawasilishwa Ofisi ya Tume Huru ya Uchaguzi kwaaajili ya uteuzi”
JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
