TAARIFA Mpya Kwa Waombaji Mikopo HESLB 2025/2026

TAARIFA Mpya Kwa Waombaji Mikopo HESLB 2025/2026
TAARIFA Mpya Kwa Waombaji Mikopo HESLB 2025/2026
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inapenda kuwafahamisha Waombaji wa Mikopo na Umma kwa ujumla kuwa tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maombi ya mikopo imesogezwa mbele kutoka tarehe 31 Agosti hadi tarehe 14 Septemba, 2025.
Hatua hii imechukuliwa ili kuwapa fursa wale ambao kwa sababu mbalimbali hawakuweza kuwasilisha maombi ya mikopo katika muda uliokuwa umepangwa.
Hadi kufikia tarehe 31 Agosti, 2025, jumla ya maombi ya mikopo 157,309 yameshapokelewa kwa mwaka wa masomo 2025/2026.
Idadi hiyo ni ongezeko la 5% ikilinganishwa na maombi 150,530 yaliyokuwa yamepokelewa katika kipindi kama hiki mwaka jana, 2024/2025.
Aidha, maombi 960 ya ‘Samia Scholarship’ yameshapokelewa ikilinganishwa na maombi 742 yaliyokuwa yamepokelewa mwaka 2024/2025, ikiwa ni ongezeko la 29%.
Itakumbukwa kuwa, Bodi ilianza kupokea maombi ya mikopo ya wanafunzi kwa njia ya mtandao kuanzia tarehe 15 Juni, 2025.
Kupitia tangazo hili, waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2025/2026 ambao wamejisajili lakini hawajakamilisha, wanashauriwa kukamilisha na kuwasilisha maombi yao ya mikopo ndani ya muda ulioongezwa.
Bodi hiyo inapenda kusisitiza kuwa hakutakuwa na muda mwingine wa nyongeza baada ya tarehe 14 Septemba, 2025.
JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?KUTUMA MAOMBI BOFYA HAPA
Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.

Namshukuru mungu
HESHIMA ! KWA MAJINA NGUSA JOHN JOSEPH
UJUMBE : TUNASHUKURURU SANA KWA NIABAA YA WALE WOTE AMBAO TUNATUMA MAOMBI KWA MWAKA HUU TULIOKWISHA KUTUMA NA AMBAO WANAENDELEA KUTUMA
KWA KUTUPA NAFASI HII YA KUONGEZEWA MUDA IKIONESHA DHAHILI HALI YA KUTHAMIN NA KUTUJALI
IKAWE KHERI KATIKA MAJUKUMU YENU MUNGU AWATIE WEPESI NA JUHUDI KATIKA KULIJENGA TAIFA
AHSANTENI SANA