JINSI ya Kupata Loss report Online bila kwenda Kituo Cha Polisi

Filed in Makala by on 01.09.2025 0 Comments
Share This Post
JINSI ya Kupata Loss report Online bila kwenda Kituo Cha Polisi

JINSI ya Kupata Loss report Online bila kwenda Kituo Cha Polisi

JINSI ya Kupata Loss report Online bila kwenda Kituo Cha Polisi

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Loss Report ni taarifa ya upotevu wa Mali au nyaraka ambayo hutolewa na Jeshi la Polisi nchini Tanzania mara mwananchi anapotoa taarifa ya upotevu wa mali ili aweze kupata msaada wa kuipata mali yake au kupewa nyingine kama vile kitambulisho, Kadi au Simu na Mali nyinginezo.

Jeshi la Polisi nchini, katika kuhakikisha linarahisisha upatikanaji wa huduma ya ‘loss report limeanzisha mfumo wa kutoa taarifa ya upotevu wa mali (Loss Report) kwa njia ya mtandao Online nchi nzima kupitia tovuti ya loss report ambayo https://lormis.tpf.go.tz.

Mfumo huu utamwezesha mwananchi kutoa taarifa za upotevu wa mali au nyaraka kwa kupitia mtandao na kuweza kupata ‘loss report’ bila kufika Kituo cha Polisi, isipokuwa kwa anayetoa taarifa ya upotevu wa kitabu cha kumiliki silaha, kadi ya gari, hati ya kiwanja au shamba, huyu itamlazimu kufika kituo cha polisi.

Kupitia mfumo huo mwananchi anaweza kutoa taarifa ya kupotelewa mali au nyaraka kwa kutumia kompyuta au simu yenye ‘internet’.

Taarifa hiyo inaweza kutolewa mwananchi akiwa mahali popote ilimradi awe na kifaa cha kielektroniki chenye mtandao atakachotumia kutolea taarifa.

Ili kutoa taarifa bila kufika kituoni inambidi mwananchi kutembelea tovuti ambayo ni https://lormis.tpf.go.tz inayopatikana kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza.

Mwananchi akishaingia kwenye tovuti atabonyeza kitufe cha Sajili Mali Iliyopotea na ataendelea kujaza fomu atakayoipata.

Baada ya kujaza fomu hiyo mwananchi atatakiwa kufanya malipo ya Tsh 1,000 Kwa Control Number itayotolewa na Mfumo ambayo inaanzia na 99108

Malipo hayo yanafanyika kupitia mfumo wa kielektroniki yaani Government electronic Payment Gateway (GePG) kwenye mitandao yote ya simu na kwenye Benki.

Mwananchi akilipa kwa mitandao ya simu za mkononi atachagua namba 4 (lipa bili), kisha atachagua namba 5 (Malipo ya Serikali) na kisha ataingiza namba ya malipo (Control number) yake na kulipa kiasi cha 1,000/=

Baada ya Kulipia Mwananchi atarudi kwenye mfumo wa Loss report na kuchagua sehemu iliyoandikwa Tafuta Taarifa/Thibitisha Taarifa Kisha ataweka Ile Control Number na atadownlod PDF ya Loss report yake kwaajili ya Matumizi.

Ukiwa unahitaji kutengenezewa Loss report wasiliana nasi hapa

Pia unaweza kuscan QR Code hapa chini.

JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?
Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, GROUP NO 2 HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA, GROUP NO 3 HAPA, GROUP NO 4 HAPA


Share This Post

Tags: , , , , ,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *