MAGAZETI ya Leo Jumatatu 01 September 2025

Filed in Magazetini Leo by on 01.09.2025 0 Comments
Share This Post
MAGAZETI ya Leo Jumatatu 01 September 2025

MAGAZETI ya Leo Jumatatu 01 September 2025

MAGAZETI ya Leo Jumatatu 01 September 2025

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Watu wawili wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa baada ya kutokea mlipuko eneo la Kichemuchemu, Kata ya Magomeni, wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Jumapili Agosti 31, 2025, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Salim Morcase amesema tukio hilo limetokea saa moja asubuhi.

Amewataja waliofariki dunia ni Dotto Mrisho, fundi wa kuchomelea na mkazi wa Kichemuchemu, pamoja na Said Ramadhani, mkazi wa Sanzale, wilayani Bagamoyo.

Kamanda huyo amesema uchunguzi wa awali umeonesha mlipuko huo umetokana na kipande cha chuma kilichokuwa kinakatwa na Mrisho wakati akifanya shughuli zake.

“Kwa sasa tunaendelea na uchunguzi zaidi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama ili kubaini hasa chanzo cha mlipuko huo, na tutatoa taarifa kamili mapema iwezekanavyo,” amesema Morcase.

Pia, ametoa wito kwa wananchi kuepuka kukata au kuchomelea vyuma ambavyo hawana uhakika navyo, ikiwamo mitungi ya gesi na vifaa vyenye umbo la duara vilivyozibwa, kwa kuwa, vinaweza kusababisha madhara makubwa.

JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?
Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, GROUP NO 2 HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA, GROUP NO 3 HAPA, GROUP NO 4 HAPA


Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *