NAFASI 35 Za Walimu Tunduru District Council

Filed in Ajira by on 01.09.2025 0 Comments
Share This Post
NAFASI 35 Za Walimu Tunduru District Council

NAFASI 35 Za Walimu Tunduru District Council

NAFASI 35 Za Walimu Tunduru District Council

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru anapenda kuwatangazia watanzania wote wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi za Mkataba za Mwalimu B, Kwa Masomo ya Biashara (Nafasi III 31), Kiingereza (Nafasi 02) na Historia (Nafasi 02).

Hivyo anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi hizo kama zilizoanishwa hapa chini.

✅MWALIMU DARAJA LA III B-MASOMO YA BIASHARA (NAFASI 31)

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kuandaa azimio la kazi, maandalio ya masomo, nukuu za masomo na Mpango wa Kazi wa majukumu mengine aliyokabidhiwa.
  • Kutengeneza na Kufaraghua zana za kufundishia na kujifunzia.
  • Kufundisha, kufanya Tathmini na kutunza kumbukumbu za Maendeleo ya Wanafunzi.
  • Kusimamia na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi Shuleni na Darasani.
  • Kusimamia malezi ya wanafunzi Kiakili, Kimwili, Kiroho na kutoa ushauri nasaha na unasihi.
  • Kutoa ushauri wa Kitaalamu na kitaaluma kuhusu maendeleo ya Elimu.
  • Kusimamia na utunzaji wa vifaa na mali za Shule.
  • Kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wa Shule kulingana na majukumu ya Shule.

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye Stashahada ya Elimu (Diploma in Education) yenye somo la kufundishia la Biashara au Usimamizi wa Biashara (Commerce/Bookkeeping/ Business Administration Business studies) AU Stashahada isiyo ya Ualimu/Elimu yenye somo la kufundishia la Biashara au usimamizi wa biashara (Commerce/ Bookkeeping/ Business Administration na Business Studies) kutoka Vyuo vinavyotambulika na Serikali.

MSHAHARA: Mwalimu wa Mkataba atalipwa posho ya Tsh.300,000/= kwa mwezi.

✅MWALIMU DARAJA LA IIIB-MASOMO YA KIINGEREZA (NAFASI 02)

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kuandaa azimio la kazi, maandalio ya masomo, nukuu za masomo na Mpango wa Kazi wa majukumu mengine aliyokabidhiwa.
  • Kutengeneza na Kufaraghua zana za kufundishia na kujifunzia.
  • Kufundisha, kufanya Tathmini na kutunza kumbukumbu za Maendeleo ya Wanafunzi.
  • Kusimamia na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi Shuleni na Darasani.
  • Kusimamia malezi ya wanafunzi Kiakili, Kimwili, Kiroho na kutoa ushauri nasaha na unasihi.
  • Kutoa ushauri wa Kitaalamu na kutaaluma kuhusu maendeleo ya Elimu.
  • Kusimamia na utunzaji wa vifaa na mali za Shule.
  • Kazi nyingine atakazopangwa na Mkuu wa Shule kulingana na majukumu ya Shule

SIFA ZA KUAJIRIWA
Kuajiriwa mwenye Stashahada ya Elimu (Diploma in Education) yenye somo la kufundishia la Kiingereza kutoka vyuo vinavyotambulika na Serikali.

MSHAHARA: Mwalimu wa Mkataba atalipwa posho ya Tsh.300,000/= kwa mwezi.

✅MWALIMU DARAJA LA IIIB-MASOMO YA HISTORIA (NAFASI 02)

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kuandaa azimio la kazi, maandalio ya masomo, nukuu za masomo na Mpango wa Kazi wa majukumu mengine aliyokabidhiwa.
  • Kutengeneza na Kufaraghua zana za kufundishia na kujifunzia.
  • Kufundisha, kufanya Tathmini na kutunza kumbukumbu za Maendeleo ya Wanafunzi.
  • Kusimamia na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi Shuleni na Darasani.
  • Kusimamia malezi ya wanafunzi Kiakili, Kimwili, Kiroho na kutoa ushauri nasaha na unasihi.
  • Kutoa ushauri wa Kitaalamu na kitaaluma kuhusu maendeleo ya Elimu.
  • Kusimamia na utunzaji wa vifaa na mali za Shule.
  • Kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wa Shule kulingana na majukumu ya Shule.

SIFA ZA KUAJIRIWA
Kuajiriwa mwenye Stashahada ya Elimu (Diploma in Education) yenye somo la kufundishia la Historia kutoka vyuo vinavyotambulika na Serikali.

MSHAHARA: Mwalimu wa Mkataba atalipwa posho ya Tsh.300,000/= kwa mwezi.

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI WOTE.

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na usiozidi miaka 45.
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswakuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira Ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya ajira katika Utumishi wa Umma.
  • Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na anuani ya barua pepe (Email Address) pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificate – Cheti cha Mtihani wa Kidato cha nne na cha Sita, Computer Certificate, Vyeti vya Kitaaluma (Proffessional Certificate from Respective Boards).
  • Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTVET).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Waombaji watakaowasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.
  • Wasailiwa ambao majina yao yanatofautiana katika nyaraka zao wanapaswa kuwasilisha Hati ya Kiapo cha Kubadili Jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi.

Barua zote zitumwe kwa njia ya posta kwa:
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
48 Barabara ya Nalasi, S. L. P 275, 57682
Tunduru.

Mwisho wa Kutuma Maombi ni tarehe 10 Septemba, 2025.

JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?
Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, GROUP NO 2 HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA, GROUP NO 3 HAPA, GROUP NO 4 HAPA

Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *