MATOKEO ya Mitihani ya CBA, UANAGENZI na NABE Msimu wa Mei 2025

MATOKEO ya Mitihani ya CBA, UANAGENZI na NABE Msimu wa Mei 2025
MATOKEO ya Mitihani ya CBA, UANAGENZI na NABE Msimu wa Mei 2025
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) iliendesha Mitihani ya Taifa ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa Msimu wa Mwezi Juni, 2025 ikiwa ni hatua za kutathmini umahiri uliopatikana katika kipindi husika cha mafunzo katika ngazi ya 1, 2 na 3.
Mitihani hiyo ilihusisha jumla ya watahiniwa 9,910 waliofanya mitihani katika programu zifuatazo: Programu ya Kupima Umahiri (CBA), Programu maalum ya Uanagenzi Pacha (DATS), Programu ya Mafunzo ya Biashara (NABE) na Programu ya Uanagenzi katika fani za madini (IMTT). Wastani wa ufaulu kwa programu zote nne (4) ni asilimia 74.5.
MATOKEO
VETA inawatangazia wahitimu na wananchi kwa ujumla kuwa matokeo ya mitihani hiyo yako tayari.
Matokeo yanapatikana kwenye vyuo vyote vya VETA nchi nzima au kupitia tovuti ya VETA
MCHANGANUO WA MATOKEO HAYO
MATOKEO YA MITIHANI YA UFUNDI STADI KATIKA MFUMO WA CBA
(COMPETENCE BASED ASSESSMENT)
Mchanganuo wa ufaulu kwa kila ngazi ni kama ifuatavyo:
- Matokeo ya Mitihani ya Ufundi Stadi Ngazi ya Kwanza (Level 1)
Jumla ya watahiniwa 807 walifanya mitihani ya Ufundi Stadi kwa mfumo wa CBA katika ngazi ya kwanza ambapo watahiniwa 298 (36.9%) walifaulu mitihani kati
yao, wakiume walikuwa 223 (39.6%) na wakike ni 75 (30.7%). - Matokeo ya Mitihani ya Ufundi Stadi Ngazi ya Pili (Level 2)
Jumla ya watahiniwa 3,127 walifanya mitihani ya Ufundi Stadi kwa mfumo wa CBA katika ngazi ya pili ambapo watahiniwa 2,224 (71.1%) walifaulu mitihani kati yao,
wakiume walikuwa 1,346 (73.5%) na wakike ni 786 (60.6%). - Matokeo ya Mitihani ya Ufundi Stadi Ngazi ya Tatu (Level 3) Jumla ya watahiniwa 5,795 walifanya Mitihani ya Ufundi Stadi kwa mfumo wa CBA katika Ngazi ya Tatu ambapo jumla ya watahiniwa 4,785 sawa na asilimia 82.6 walifaulu, kati yao wakiume ni 3,840 (83.4%) na wakike ni 1,686 (81.2%).
- Watahiniwa wanaopaswa kurudia mitihani kwa ngazi zote Watahiniwa 2,422 (24.9%) kati ya 9,729 waliofanya Mitihani ya CBA kwa Ngazi ya 1, 2 na ya 3 wanapaswa kurudia Mitihani hiyo.
MATOKEO YA MITIHANI YA TAIFA YA PRAGRAMU YA ELIMU YA BIASHARA –
NABE (NATIONAL BUSINESS EXAMINATIONS)
Jumla ya watahiniwa 107 walifanya Mitihani ya Taifa ya Elimu ya Biashara katika hatua ya 1, 2 na 3, ambapo jumla ya watahiniwa 24 (22.4%) walifaulu mitihani.
Kati yao, wakiume ni 7 (53.8%) na wakike ni 17 (18.1%).
Hivyo watahiniwa 83 (77.6 %) wanapaswa kurudia Mitihani hiyo.
PROGRAMU YA UANAGENZI PACHA (DUAL APPRENTICESHIP TRAINING
SYSTEM)
Jumla ya watahiniwa 31 walifanya mitihani ya Programu ya Uanagezi Pacha
ambapo 24 sawa na asilimia 77.4 walifaulu, kati yao wakiume 1 sawa na asilimia 100 na wakike 23 sawa na asilimi 76.7.
PROGRAMU RASMI YA UANAGENZI KWA FANI ZA MADINI (INTERGRATED
MINING TECHNICAL TRAINING- IMTT)
Jumla ya watahiniwa 43 walifanya mitihani ya Programu ya Uanagenzi kwaajili ya Ufundi kwenye shughuli za Uchimbaji Madini (IMTT), ambapo watahiniwa 26 sawa na asilimia 60.5 walifaulu mitihani, kati yao wakiume 23 sawa na asilimia 60.5 na wakike 3 sawa na asilimia 60.0.
Kupata matokeo ya mitihani ya CBA, Uanagenzi na NABE kwa msimu wa Mei, 2025 Donwload PDF hapa chini.
JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?MATOKEO YA MITIHANI YA CBA, UANAGENZI NA NABE KWA MSIMU WA MEI 2025
Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, GROUP NO 2 HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA, GROUP NO 3 HAPA, GROUP NO 4 HAPA
Tags: MATOKEO ya Mitihani ya CBA, UANAGENZI na NABE Msimu wa Mei 2025
