MATOKEO ya Uchaguzi wa Udahili wa Pamoja (CAS) Kozi za Afya na Sayansi Shirikishi 2025/2026 Awamu ya Pili

Filed in Elimu by on 02.09.2025 0 Comments
Share This Post
MATOKEO ya Uchaguzi wa Udahili wa Pamoja (CAS) Kozi za Afya na Sayansi Shirikishi 2025/2026 Awamu ya Pili

MATOKEO ya Uchaguzi wa Udahili wa Pamoja (CAS) Kozi za Afya na Sayansi Shirikishi 2025/2026 Awamu ya Pili

MATOKEO ya Uchaguzi wa Udahili wa Pamoja (CAS) Kozi za Afya na Sayansi Shirikishi 2025/2026 Awamu ya Pili

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

MATOKEO YA UCHAGUZI WA UDAHILI KUPITIA MFUMO WA UDAHILI WA PAMOJA (CAS) KWA KOZI ZA AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI KWA MWAKA WA MASOMO 2025/2026 – AWAMU YA PILI

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) linautaarifu umma kuwa matokeo ya uchaguzi wa awamu ya pili kwa waombaji wa programu za Afya na Sayansi Shirikishi kwa mwaka wa masomo 2025/2026 yametangazwa rasmi tarehe 1 Septemba, 2025.

Baraza hilo liliratibu udahili wa wanafunzi awamu ya pili katika kozi mbalimbali za afya na sayansi shirikishi kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) kwa mwaka wa masomo 2025/2026.

Jumla ya waombaji 15,526 waliwasilisha maombi yao kupitia CAS.

Jumla ya waombaji 15,526 walikamilisha maombi yao kwa kuchagua vyuo/programu walizozipenda.

Jumla ya waombaji 12,988 walikuwa na sifa kwenye programu walizoomba na jumla ya waombaji 2,538 hawakuwa na sifa kwenye programu walizoomba.

Jumla ya waombaji 10,476 wamechaguliwa kujiunga kwenye vyuo vinavyotoa programu mbalimbali za Afya na Sayansi Shirikishi ambapo wanawake ni 5,186 (49.5%) na wanaume 5,290 (50.5%).

Waombaji 330 walichaguliwa kwenye vyuo vya serikali na waombaji 10,146 katika vyuo visivyo vya serikali.

Aidha, waombaji waliokuwa na sifa lakini hawakuchaguliwa kutokana na ushindani katika programu na vyuo walivyoomba, wanashauriwa kuwasilisha maombi ya kujiunga na vyuo vyenye nafasi kupitia dirisha la awamu ya tatu kwa kutumia Mfumo wa Udahili wa Pamoja.

Waombaji wote wanashauriwa kuangalia matokeo ya uchaguzi wa udahili kupitia tovuti ya Baraza hilo kwa kubonyeza CAS Selection 2025

Baraza linautaarifu umma kuwa dirisha la awamu ya tatu la udahili litafunguliwa rasmi kuanzia tarehe 2 hadi 26 Septemba, 2025 na matokeo ya uchaguzi wa udahili yatatangazwa tarehe 5 Oktoba, 2025

Aidha, wale wanaohitaji kubadilisha programu au chuo, dirisha la uhamisho litakuwa wazi kuanzia tarehe 2 hadi 26 Septemba, 2025, hivyo watumie dirisha hili kukamilisha maombi hayo kupitia tovuti ya Baraza kwa kubonyeza kwenye akaunti yake aliyotumia kuomba na kuchaguliwa.

JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?
Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, GROUP NO 2 HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA, GROUP NO 3 HAPA, GROUP NO 4 HAPA


Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *