MAJINA ya Waliochaguliwa Chuo Zaidi ya Kimoja au Programu zaidi ya moja 2025/2026

MAJINA ya Waliochaguliwa Chuo Zaidi ya Kimoja au Programu zaidi ya moja 2025/2026
MAJINA ya Waliochaguliwa Chuo Zaidi ya Kimoja au Programu zaidi ya moja 2025/2026
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inaufahamisha umma, Taasisi za Elimu ya Juu na wadau wa Elimu ya Juu ndani na nje ya nchi kuwa Awamu ya Kwanza ya udahili wa Shahada ya Kwanza katika Taasisi za Elimu yavJuu nchini kwa mwaka wa masomo 2025/2026 imekamilika.
Majina ya waliodahiliwa katika awamu hii yanatangazwa na vyuo husika.
Katika Awamu ya Kwanza ya udahili, jumla ya waombaji 146,879 wametuma maombi ya kujiunga katika vyuo 88 vilivyoidhinishwa kudahili wanafunzi katika Shahada ya Kwanza.
Aidha, jumla ya programu 894 zimeruhusiwa kudahili ikilinganishwa na programu 856 mwaka 2024/2025, ikiwa ni ongezeko la programu 38 za masomo. Vilevile kwa upande wa nafasi za udahili, mwaka huu kuna jumla ya nafasi 205,652 ikilinganishwa na nafasi 198,986 mwaka uliopita.
Hili ni ongezeko la nafasi 6,666 sawa na asilimia 3.3 katika programu za Shahada ya Kwanza.
Pia katika Awamu ya Kwanza ya udahili, jumla ya waombaji 116,596 sawa na asilimia 79.4 ya waombaji wote walioomba udahili, wamepata udahili kwenye vyuo walivyoomba.
Idadi ya waombaji wa udahili na watakaodahiliwa inatarajia kuongezeka katika Awamu ya Pili ya udahili.
WAOMBAJI WALIODAHILIWA KATIKA CHUO ZAIDI YA KIMOJA
Waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja wanapaswa kuthibitisha udahili wao katika chuo kimojawapo kuanzia leo tarehe 03 hadi 21 Septemba, 2025.
Uthibitisho huo unafanyika kwa kutumia namba maalum ya siri iliyotumwa kwa ujumbe mfupi kupitia namba zao za simu au barua pepe walizotumia wakati wa kuomba udahili.
Wale ambao hawatapata kwa wakati ujumbe huo, wanashauriwa kuingia kwenye mifumo ya udahili ya vyuo walivyodahiliwa na kuomba kutumiwa ujumbe mfupi wenye namba maalum ya siri ili kuweza kujithibitisha katika chuo husika.
Aidha, uthibitisho wa udahili ufanyike kupitia akaunti ambayo muombaji
alitumia wakati wa kuomba udahili. Kwa urahisi wa rejea, orodha ya majina
ya waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja yameoorodheshwa hapa chini.
JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?Orodha ya Waombaji waliodahiliwa zaidi ya Chuo kimoja au Programu zaidi ya moja 2025/2026
Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, GROUP NO 2 HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA, GROUP NO 3 HAPA, GROUP NO 4 HAPA
Tags: MAJINA ya Waliochaguliwa Chuo Zaidi ya Kimoja au Programu zaidi ya moja 2025/2026

Not yet opened