TCU Kufunguliwa Kwa awamu ya Pili ya Udahili 2025/2026

TCU Kufunguliwa Kwa awamu ya Pili ya Udahili 2025/2026
TCU Kufunguliwa Kwa awamu ya Pili ya Udahili 2025/2026
Tume inatangaza kuwa Awamu ya Pili ya udahili wa Shahada ya Kwanza kwa mwaka wa masomo 2025/2026 imeanza leo tarehe 03 hadi 21 Septemba, 2025.
Tume inawaasa waombaji ambao hawakuweza kutuma maombi ya udahili au hawakuweza kupata nafasi ya kudahiliwa katika Awamu ya Kwanza kutokana na sababu mbalimbali, watumie fursa hii vizuri kwa kutuma maombi yao ya udahili kwenye vyuo wanavyovipenda.
Aidha, Tume inaelekeza Vyuo vya Elimu ya Juu nchini kutangaza programu
ambazo bado zina nafasi.
Waombaji udahili na vyuo wanapaswa kuzingatia utaratibu wa udahili wa Awamu ya Pili kama ilivyooneshwa kwenye kalenda ya udahili iliyoko katika tovuti ya TCU (www.tcu.go.tz).
WITO KWA WAOMBAJI UDAHILI Waombaji udahili wa Shahada ya Kwanza wanakumbushwa kuwa masuala yote yanayohusu udahili au kujithibitisha katika chuo kimoja yawasilishwe moja kwa moja kwenye vyuo husika.
Kwa wale ambao watapata changamoto katika kujithibitisha, vyuo vyote vimeelekezwa kupokea taarifa zao na kutafuta ufumbuzi wa haraka kwa kuzingatia miongozo na taratibu zilizowekwa.
JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?Soma Tangazo la Kukamilika kwa awamu ya Kwanza na kufunguliwa kwa awamu ya Pili ya Udahili 2025/2026
Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
