MAGAZETI ya Leo Jumamosi 06 September 2025

MAGAZETI ya Leo Jumamosi 06 September 2025
MAGAZETI ya Leo Jumamosi 06 September 2025

Serikali ya Rwanda kwa kushirikiana na Kampuni ya Ujenzi ya China ya Road and Bridge Corporation (CRBC) wamezindua Ndege taksi ya umeme inayojiendesha yenyewe ikiwa ni ya kwanza Barani Afrika ambayo imefanya safari yake ya kwanza Septemba 4, 2025 Nchini humo.
Maonyesho ya moja kwa moja ya ndege hiyo taxi iliyopewa jina la EHang EH216-S isiyo na rubani, yamefanyika Alhamisi Septemba 4 katika Mkutano wa Kilele wa Usafiri wa Anga Afrika.
“Rwanda inajenga mustakabali ambapo Miji yetu itaunganishwa zaidi na uchumi wetu kuwa wenye nguvu kupitia suluhisho la usafiri bunifu, kupitia ushirikiano huu wa kihistoria tunaonesha si tu mustakabali wa anga bali pia dhamira yetu ya kujenga mazingira salama na ya kisasa ya kisheria kwa usafiri wa anga wa kisasa” -Waziri wa Miundombinu, Jimmy Gasore.
Kupitia ushirikiano wa Rwanda na CRBC ambao ni wazoefu wa kimataifa wa maswala ya Uhandisi, Rwanda inalenga kujenga mfumo mpya wa usafiri wa anga wa kisasa ambao unalenga kupunguza msongamano wa magari na kuunganisha jamii na kutoa suluhisho endelevu za usafiri Nchini humo na barani Afrika ikiwa na lengo la kuwapa Wadau na Wasimamizi wa usafiri kielelezo cha moja kwa moja cha matumizi ya teknolojia ya usafiri wa anga ya kisasa.
JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
