MAGAZETI ya Leo Ijumaa tarehe 12 September 2025

MAGAZETI ya Leo Ijumaa tarehe 12 September 2025
MAGAZETI ya Leo Ijumaa tarehe 12 September 2025

Watu sita wamefariki Dunia papo hapo na mmoja kujeruhiwa baada ya gari walikokuwa wakisafiria kugonga kwa nyuma gari lililokuwa limeegeshwa barabarani baada ya kuharibika.
Ajali hiyo imetokea katika Kijiji cha Buganjo wilayani Rorya wakati gari aina ya Toyota Succeed likiwa limebeba watu saba likiwa linatoka mjini Tarime kuelekea Kijiji cha Busurwa wilayani Rorya, liligonga kwa nyuma gari aina ya Fuso liliokuwa limeegeshwa pembezoni mwa barabara baada ya kuharibika.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya, Mark Njera ameeleza ajali hiyo imetokea leo Septemba 11,2025 saa 11 alfajiri.
“Gari aina ya Succeed iliyokuwa inatoka Tarime kuelekea Rorya iligonga kwa nyuma gari aina ya Fuso lililokuwa limeegeshwa pembezoni mwa barabara baada ya kuharibika,” amesema na kuongeza jeshi hilo linaendelea na uchunguzi kubaini kiini cha ajali hiyo.
Amesema majina ya watu hao hayajatambulika na miili yao imehifadhiwa katika Hospitali ya Utegi wilayani Rorya huku hali ya majeruhi ikiwa ni mbaya.
Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
