MAGAZETI ya Leo Jumamosi tarehe 13 September 2025

MAGAZETI ya Leo Jumamosi tarehe 13 September 2025
MAGAZETI ya Leo Jumamosi tarehe 13 September 2025
Rais wa Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania (TPBA), Bavoo Junus, amewashauri wananchi kuepuka kujadili masuala ya kisheria bila kuwa na uelewa wa kutosha, akisema hatua hiyo imekuwa ikisababisha upotoshaji mkubwa unaoweza kudhoofisha imani ya jamii kwa taasisi za sheria.
Akizungumza Ijumaa, Septemba 12, 2025, jijini Dodoma, Junus amesema kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakitoa tafsiri potofu za sheria katika majukwaa mbalimbali bila kuwa na utaalamu wowote wa taaluma hiyo, jambo ambalo linaweza kuwachanganya wananchi na hata kuchochea vurugu.
“Hakuna mtu nje ya Serikali anayeijua sheria kuliko sisi. Sisi ndio hupitia, kuchambua na kuhakikisha kila sheria inazingatia masilahi ya Taifa kabla haijafika popote. Niwaombe wasio na uelewa juu ya sheria waache kupotosha umma,” amesema Junus.
JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
