ARAJIGA apewa Yanga vs Simba 16 September 2025

ARAJIGA apewa Yanga vs Simba 16 September 2025
ARAJIGA apewa Yanga vs Simba 16 September 2025
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limemtangaza mwamuzi Ahmed Arajiga, kuwa mwamuzi wa kati kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii utakao wakutanisha Yanga dhidi ya Simba.
Ofisa Habari wa TFF Clifford Ndimbo, amesema kuwa Arajiga atakuwa mwamuzi wa kati kwenye mchezo huo, akisaidiwa na Mohammed Mkono, atakayekuwa mwamuzi msaidizi wa kwanza na Kassim Mpanga, atakayekuwa mwamuzi namba msaidizi namba mbili.
Aidha Ndimbo amesema, mwamuzi wa nne atakuwa Ramadhan Kayoko kwenye mchezo huo ambao utapigwa kesho Jumanne tarehe 16 September 2025 kwenye Uwanja Benjamin Mkapa
Rekodi zinaonyesha hii itakuwa ni Dabi ya tano kwa mwamuzi huyo kutoka Babati kuamua mchezo huo.
Arajiga anaipokea Dabi hiyo kutoka kwa wamuzi wa Misri, ambao walichezesha mchezo wa mwisho baina ya timu hizo, kwenye kufunga msimu uliopita wa Ligi, ambapo Simba ilichezea kipigo cha mabao 2-0.

ARAJIGA apewa Yanga vs Simba 16 September 2025
Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
