LUHAGA Mpina aondolewa kwenye Orodha ya Wagombea Urais 2025

itel LUHAGA Mpina aondolewa kwenye Orodha ya Wagombea Urais 2025
LUHAGA Mpina aondolewa kwenye Orodha ya Wagombea Urais 2025
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imemuengua mgombea urais kwa tiketi ya ACT-Wazalendo, Luhaga Mpina.
Taarifa kwa umma iliyotolewa leo, Septemba 15,2025, iliyosianiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa INEC, Ramadhani Kailima imesema jina lake limeondolewa kutokana na pingamizi la Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari.
“Tume imekubali pingamizi lililowasilishwa na Hamza Saidi Johari Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya uteuzi wa Luhaga Mpina kuwa mgombea wa kiti cha Rais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo.
Hivyo, jina la Luhaga Mpina, mgombea wa kiti cha Rais kupitia Chama cha ACT Wazalendo limeondolewa kwenye orodha ya wagombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.”
Aidha, INEC imetupa mapingamizi ya vyama vya AAFP na NRA.

Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, GROUP NO 2 HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA, GROUP NO 3 HAPA, GROUP NO 4 HAPA
Tags: LUHAGA Mpina aondolewa kwenye Orodha ya Wagombea Urais 2025
