NAFASI Za Kazi Unitrans Tanzania Limited

NAFASI Za Kazi Unitrans Tanzania Limited
NAFASI Za Kazi Unitrans Tanzania Limited
Kampuni ya Unitrans Tanzania inakaribisha maombi kutoka kwa waombaji wenye sifa na ujuzi stahiki kujaza nafasi zifuatazo;
Dereva wa lori – Nafasi 70 Eneo la kazi: Kilombero Aina ya mkataba: Msimu
MAJUKUMU
- Kufanyakazi ya kusomba miwa kutoka mashambani kwenda viwandani.
- Na majukumu mengine yanayoendana na taaluma ya udereva.
SIFA ZA MWOMBAJI
- Awe na ufahamu wa Sheria ya Usalama Barabarani na kanuni zake.
- Awe na leseni halali ya daraja E.
- Awe anajua kusoma na kuandika.
- Awe na cheti halali cha mafunzo ya udereva wa Magari Makubwa – Rigid au HGV-Magari ya Kuvuta Trela (GOOD TRUCK DRIVING-RIGID or HGV (Pulling Trucks) kutoka katika chuo kinachotambulika na serikali.
- Awe na uzoefu wa kuendesha lori usiopungua miaka 2
- Awe na barua ya uhakiki wa leseni kutoka Mkuu wa polisi kitendo cha barabarani Awe na umri usiopungua miaka 25 na usiozidi miaka 45.
- Awe tayari kufanya kazi usiku.
- Barua za maombi ziambatanishwe na nakala ya namba ya Nlipa kodi (TIN), NIDA, Cheti cha mafunzo Pamoja na CV.
Maombi yatumwe kwenye anwani ifuatayo; Meneja rasilimali watu, Unitrans Tanzania Ltd, PO Box 50, Kidatu.
Au ziletwe ofisi za Unitrans Tanzania Limited, zikabidhiwe kwa mlinzi getini.
Kwa kutuma maombi ya kazi hii, mwombaji anakubali kwamba taarifa zake binafsi zitahifadhiwa na kutumika na kampuni kwa madhumuni ya mchakato wa ajira pekee na kwa kuzingatia kanuni na taratibu za sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.
Mwisho wa Kutuma maombi ni tarehe 18/09/2025.
JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
