NAFASI Za Kazi Sumbawanga District Council

NAFASI Za Kazi Sumbawanga District Council
NAFASI Za Kazi Sumbawanga District Council
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga anawatangazia Watanzania wenye sifa ya kufanya kazi Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kuomba nafasi kumi na tatu (13) zilizo tajwa hapo chini, baada ya kupokea kibali cha mwaka wa fedha 2024/2025 chenye Kumb.Na. FA.97/228/01/A/25 cha tarehe 29/04/2025 na kibali cha mwaka wa fedha 2023/2024 chenye Kumb.Na.FA.97/228/01/06 cha tarehe 06/04/2023 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Raisi Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – NAFASI 03
MAJUKUMU YA KAZI
- Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na Siri.
- Kupokea Wageni na kuwasaili shida zao na kuwaelekeza wanapoweza kusaidiwa.
- Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine.
- Kufuata majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji majukumu ya kazi.
- Kupokea majalada na kusambaza kwa Maafisa walio katika Divisheni/Vitengo au sehemu husika.
- Kukusanya, kutunza, na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinakohusika.
- Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya Vikao mbalimbali.
- Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya Ofisi.
- Kutekeleza Shughuli zingine utakazopangiwa na Mwajiri.
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa kwa wahitimu wa kidato cha IV/VI wenye Stashahada (Diploma) – NTA Level 6 katika fani ya Uhazili na awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata mafunzo ya programu za Kompyuta za Ofisi kama vile :- Word, Excel, Power point, Internet, E-mail na Publisher kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
MSHAHARA: Mshahara utaanzia Ngazi ya TGS C – 1.
✅DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 08
MAJUKUMU YA KAZI
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari Kuwapeleka Watumishi sehemu mbalimbali kwenye safari za Kikazi Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
- Kutunza na kuandika daftari la safari “log book” kwa safari zote.
- Kukusanya na kusambaza au kuasafirisha nyaraka na vitu mbalimbali Kufanya Usafi wa gari.
- Kutekeleza Shughuli zingine atakazopangiwa na Mwajiri.
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa kwa wahitimu wa kidato cha IV/VI na kupata Cheti, awe na Leseni Daraja la ‘C’ au ‘E’ ya uendeshaji, awe amehudhuria mafunzo ya Msingi ya uendeshaji magari (Basic Ufundi (VETA) au Chuo Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha Mafunzo ya chochote kinachotambuliwa na Serikali na wenye uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua Mwaka mmoja bila kusababisha ajali.
MSHAHARA: Mshahara utaanzia Ngazi ya TGS B – 1.
✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI 02
MAJUKUMU YA KAZI
- Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye regista (incoming correspondence register).
- Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasisi (outgoing correspondence register).
- Kutafuta kumbukumbu /nyaraka/majalada yanayohitajika na Watendaji.
- Kusambaza majalada kwa Watendaji (action Officers).
- Kupokea majalada yanayorudi masjala toka kwa Watendaji.
- Kurudisha majalada kwenye shubaka/kabati la majalada (racks /filling cabinets) au mahali pengine yanapohifadhiwa.
- Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya taasisi (file tracking).
- Kutekeleza Shughuli zingine utakazopangiwa na Mwajiri.
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa kwa wahitimu wa kidato cha IV/VI wenye Stashahada (Diploma) – NTA Level 6 katika mojawapo wa fani za Utunzaji wa Kumbukumbu kama vile Masjala, kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na wenye ujuzi wa kutumia kompyuta.
MSHAHARA: Mshahara utaanzia Ngazi ya TGS C – 1.
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 45, isipokuwa kwa wale wenye ajira Serikalini tu inaweza ikawa zaidi ya miaka 45. 2.
- Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa.
- Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detailed CV) yenye anuani, namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini watatu (3) wa kuaminika na anuani ya barua pepe (E-mail address).
- Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya taaluma na vyeti vya kidato cha nne au sita kwa wale waliofika kiwango hicho na vyeti vya Taaluma na vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia kazi husika na viwe vimethibitishwa na Mwanasheria.
- Testimonials, Provisional results, Statement of results na hati za matokeo ya kidato cha nne na sita (form VI and form IV result slips) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimekaguliwa na kuthibitishwa na mamlaka husika (NECTA, NACTVET na TCU).
- Uwasilishaji wa sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua stahiki za kisheria.
- Maombi yaandikwe kwa mkono na muombaji kwa lugha ya Kiswahili au kiingereza.
- Waombaji wa kazi ya Dereva Daraja la II wenye Lessen Daraja E au C wanapaswa KUAMBATISHA vyeti vya Udereva vilivyo wapatia sifa za kupata madaraja husika.
- Waombaji ambao wanautofauti wa Herufi katika kitambulisho cha Taifa na vyeti vya Taaluma, kidato cha sita,kidato cha Nne na cheti cha kuzaliwa wanatakiwa kuambatisha AFFIRDAVIT (kiapo).
- Waombaji wenye majina tofauti katika vyeti vya taaluma, kuzaliwa na Nida waambatishe DEEP POLL (Hati ya usajili wa kiapo cha majina).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelezo yaliyo katika Waraka Na.CCA.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
MUHIMU:Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu,Anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga,
S.L.P 229
SUMBAWANGA
Maombi yote yatumwe kupitia mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz.
Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’.
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA SUMBAWANGA 18-09-2025
Mwisho wa Kutuma Maombi ya Kazi ni tarehe 01/10/2025
JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
