MAGAZETI ya Leo Jumapili 21 September 2025

MAGAZETI ya Leo Jumapili 21 September 2025
MAGAZETI ya Leo Jumapili 21 September 2025
UJENZI WA MELI MPYA YA MV NEW MWANZA WAKAMILIKA SAFARI YA MWANZA – BUKOBA KUFANYIKA KWA MARA YA KWANZA

Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO) inapenda kuwataarifu wananchi na wadau wote wa usafiri kwa njia ya maji kuwa mradi wa ujenzi wa meli mpya ya abiria na mizigo katika Ziwa Victoria, MV NEW MWANZA, umekamilika.
Hivyo meli hiyo itafanya safari yake ya kwanza ya kutoka Mwanza kwenda Bukoba na kutoka Bukoba kwenda Mwanza tarehe 21 hadi 22, Septemba 2025 kabla ya kuendelea na safari za kibiashara katika Ziwa Victoria.
Siku ya Jumapili ya tarehe 21 Septemba 2025, Meli ya MV New Mwanza itaondoka Bandari ya Mwanza Kusini saa 2:00 asubuhi na kuwasili Bandari ya Bukoba jioni siku hiyo.
Siku ya Jumatatu tarehe 21 Septemba 2025 Meli ya MV New Mwanza itaondoka Bandari ya Bukoba saa 3:00 asubuhi na kuwasili Bandari ya Mwanza Kusini jioni siku hiyo.
Madhumuni ya safari hii ni kuhakikisha mifumo yote ya uendeshaji wa meli inafanya kazi kwa kiwango kinachohitajika na kwa usalama wa hali ya juu.
Safari hiyo itahusisha mabaharia, wataalamu kutoka kwa Mkandarasi, maafisa wa TASHICO, pamoja na wawakilishi kutoka vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na Shirika la Uwakala wa Meli (TASAC).
Kukamilika kwa safari hii kutafungua rasmi maandalizi ya makabidhiano ya meli hiyo, ili ianze kutoa huduma za kibiashara kwa wananchi wa Kanda ya Ziwa Victoria na Tanzania pamoja na nchi jirani.
Kupatikana kwa meli hii kutaimarisha kwa kiasi kikubwa huduma za usafiri na uchukuzi kwa njia ya maji, na hivyo kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na taifa kwa ujumla.
JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
