SIMBA yaachana na Kocha Fadlu Davids

Filed in Michezo by on 22.09.2025 0 Comments
Share This Post
SIMBA yaachana na Kocha Fadlu Davids

SIMBA yaachana na Kocha Fadlu Davids

SIMBA yaachana na Kocha Fadlu Davids

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Uongozi wa klabu ya Simba umefikia makubaliano ya kusitisha mkataba na kocha Mkuu Fadlu Davids baada ya kuhudumu na timu kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Makubaliano haya ni matakwa binafsi ya kocha Fadlu kwa uongozi wa klabu hiyo.

Klabu ya Simba inamshukuru Kocha Fadlu kwa kuiongoza Simba kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita na kumalizia nafasi ya pili kwenye Ligi kuu ya NBC.

Uongozi wa klabu unamtakia kheri na baraka kocha Fadlu katika maisha yake ya soka nje Simba.

Kocha Fadlu Davids na wasaidizi wake wapo kwenye utaratibu wa kukamilisha taratibu za safari kutoka Afrika Kusini kwenda Morocco na wanatarajia kusafiri kesho kwenda Casablanca kukamilisha usajili wa miaka mitatu akianzia miwili na mmoja wa kuongeza.

Kocha huyo na wenzake wamewaaga wachezaji wa Simba pia hawajasafiri na timu kutoka Afrika Kusini kuja Tanzania.

Kabla ya kukubali ofa ya Raja kuna mambo kadhaa ambayo baadhi ya vyanzo vya taarifa vinadokeza kuwa hayakumfurahisha Fadlu Davids.

Inaelezwa Fadlu Davids hakuridhishwa na Uwanja wa MO Arena wa Mazoezi.

Katikati ya usajili baadhi ya wachezaji walioletwa alivyowakataa ilikuwa ni mwanzo wa kutetereka kwa uhusiano wake na baadhi ya viongozi.

Usajili wa timu kwenye baadhi ya maeneo haukumfurahisha kwa kiwango alichotaka.

Alitibuka nyongo zaidi kuona wanarudi KMC Complex badala ya uwanja wa Mkapa.

Simba wao wameamua kubaki kwenye weledi tu wa kimkataba, anayevunja mkataba ndiye alipe na si vinginevyo.

JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?
Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, GROUP NO 2 HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA, GROUP NO 3 HAPA, GROUP NO 4 HAPA


Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *