NAFASI Za Kazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe

Filed in Ajira by on 23.09.2025 0 Comments
Share This Post

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe anapenda kuwatangazia watanzania wote wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe kuomba nafasi za kazi za mkataba zilizotajwa hapo chini kuwasilisha maombi yao.

Nafasi Zilizotangazwa na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe ni kama ifuatavyo;

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

✅MTEKNOLOJIA MIONZI DARAJA LA II (RADIOGRAPHER II ) NAFASI 02

SIFA ZA KUAJIRIWA
Kuajiriwa mwenye Stashahada katika fani ya mteknolojia daraja la II – Radiografa kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali na ambao wamesajiliwa na baraza (Medical Radiology and Imaging Professional Council)

KAZI NA MAJUKUMU

  • Kutunza mitambo na vifaa vya Radiotherapia katika eneo lake la kazi.
  • Kutoa huduma ya vipimo kwa wagonjwa wanaoelekezwa eneo lake lake la kazi kwa mionzi sahihi.
  • Kukagua na kusimamia ubora wa mionzi inayotolewa na mitambo ya radiotherapia (Radio – therapetic quality).
  • Kusimamia watumishi walio chini yake.
  • Kutoa ushauri kuhusu kazi za radiotherapia na mionzi katika eneo lake la kazi.
  • Kuandaa vifaa vya tiba/uchunguzi na kusimamia utakasaji katika eneo la kazi (sterilization).
  • Kutoa mafunzo ya awali kwa watumishi wanaopangiwa kazi katika eneo lake la kazi.
  • Kufanya kazi nyingine atakazo pangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.

✅MUUGUZI DARAJA LA II (NURSE II) NAFASI 10

SIFA ZA KUAJIRIWA
Kuajiriwa wenye Astashahada katika fani ya Uuguzi kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali na ambao wamesajiliwa na baraza (Tanzania Nursing and Midwifery Council)

KAZI NA MAJUKUMU

  • Kufanya kazi za kiuguzi za kuhudumia wateja katika jamii, Hospitali na sehemu zote zinapotolewa huduma za afya.
  • Kusimamia na kuratibu kazi zote za wahudumu wa afya katika sehemu yake ya kazi.
  • Kukusanya takwimu na kutayarisha taarifa za utendaji wake wa kazi.
  • Kutoa huduma ya wagonjwa majumbani.
  • Kutoa ushauri nasaha
    Kutoa huduma za kinga na uzazi wa mpango.
  • Kutoa huduma za uzazi na afya ya mtoto.
  • Kuelimisha wagonjwa na jamii kuhusu matatizo yao ya kiafya.
  • Kufuatilia utunzaji wa vitendeakazi katika maeneo yake ya kazi.
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.

✅MSAIDIZI WA AFYA (HEALTH ASSISTANT) NAFASI 04

SIFA ZA KUAJIRIWA
Kuajiriwa wenye Astashahada katika fani ya wasaidizi wa afya (Health assistants) kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali

KAZI NA MAJUKUMU

  • Kufanya usafi wa vifaa vya kazi, maeneo ya kutolea huduma za afya pamoja na mazingira yanayozunguka kituo.
  • Kusaidia mgonjwa asiyejiweza kwa mfano, kumlisha, kwenda haja, usafi wa mwili, nk.
  • Kukusanya nguo chafu na kuzipeleka kufuliwa (Laundry).
  • Kupeleka sampuli za mgonjwa kwaajili ya vipimo vya maabara na kufuatilia majibu.
  • Kuwasafirisha wagonjwa kati ya idara moja na nyingine ndani ya kituo cha kutolea huduma za afya
  • Kutunza vifaa vya usafi.
  • Kupokea, kupeleka chumba cha kuhifadhi, kuosha nakutunza maiti.
  • Kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa usafi wa mazingira na mwili ili kujikinga na milipuko ya magongjwa.
  • Kufanya shughuli nyingine utakazopangiwa na kiongozi wako wa kazi.

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI WOTE

  • Awe na umri usiozidi miaka 35 na mwenye afya njema.
  • Waombaji waambatishe wasifu (Curriculum Vitae) yenye anwani sahihi, namba za simu sahihi, pamoja na majina mawili ya wadhamini (watumishi wa serikali) na namba zao za simu zinazopatikana.
  • Barua za Wadhamini wawili zikiwa na anwani zao sahihi na namba za simu.
  • Awe na vyeti husika vya Taaluma. Testimonial “provisional results” statement of results, hati ya matokeo ya kidato cha nne HAVIKUBALIKI.
  • Waombaji waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na TCU au NECTA.

Waombaji waambatanishe nakala za vyeti vifuatavyo vilivyothibitishwa;

  • Cheti cha kuzaliwa.
  • Cheti cha kuhitimu Elimu ya Kidato cha nne.
  • Cheti cha kuhitimu Elimu ya Kidato cha Sita.
  • Vyeti vya taaluma.
  • Leseni kutoka Mabaraza husika.
  • Cheti cha Kompyuta.

Maombi yote yawasilishwe kwa njia ya Posta au moja kwa moja:-
MGANGA MFAWIDHI,
HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA NJOMBE,
S. L. P 1044,
NJOMBE

Mwisho wa Kutuma Maombi ni tarehe 27/09/2025

JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?
Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, GROUP NO 2 HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA, GROUP NO 3 HAPA, GROUP NO 4 HAPA


Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *