NAFASI Za Kazi Rufiji Town Council

Filed in Ajira by on 25.09.2025 0 Comments
Share This Post
NAFASI Za Kazi Rufiji Town Council

NAFASI Za Kazi Rufiji Town Council

NAFASI Za Kazi Rufiji Town Council

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Rufiji anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi za kazi kwa kada mbili (02) katika Halmashauri hiyo baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mchanganuo ufuatao:-

✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II (OFFICE MANAGEMENT SECRETARY II) – NAFASI 06

KAZI NA MAJUKUMU

  • Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri.
  • Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao na  kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
  • Kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za mkuu wake na ratiba za kazi zingine zilizopangwa kutekelezwa katika ofisi anayofanyia kazi na kumuarifu mkuu wake kwa wakati unaohitajika.
  • Kusaidia kupokea majalada na nyaraka zinazohitajika, katika utekelezaji wa majukumu yao ya kazi.
  • Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa walio katika Idara/Kitengo/Sehemu husika.
  • Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika.
  • Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali mbalimbali.
  • Kuandaa orodha ya mahitaji mbalimbali ya ofisi.

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne au Sita wenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti cha NTA Level 6 ya Uhazili. Aidha wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kingereza maneno 100 kwa dakika na kupata mafunzo ya kompyuta katika chuo chochote kinachotambulika na Serikali katika program za kompyuta za ofisi kama vile Word, Excel, PowerPoint, Internet, Email na Publisher.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi ya mishahara ya Serikali TGS C

✅DEREVA DARAJA LA II – (DRIVER II) – NAFASI 04

KAZI NA MAJUKUMU

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
  • Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kazi.
  • Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
  • Kusambaza nyaraka mbalimbali.
    Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari.
  • Kufanya usafi wa gari.
  • Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na msimamizi wake.

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo wamefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupala madaraja husika. Wawe wamehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi ya mishahara ya Serikali TGS B

MASHARTI YA JUMLA

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na usiozidi miaka 45.
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira Ulemavu walionao kwaajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya ajira katika Utumishi wa Umma.
  • Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na anuani ya barua pepe (E-mail Address) pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika
  • Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificate Mtihani wa Kidato cha nne na cha Sita, Computer Certificate, Kitaaluma (Proffessional Certificate from Respective Boards).
  • Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTVET).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi wa kada ya Dereva II wenye leseni Daraja E au C wanapaswa KUAMBATISHA vyeti vya mafunzo ya Udereva vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Waombaji watakaowasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.
  • Wasailiwa ambao majina yao yanatofautiana katika nyaraka zao wanapaswa kuwasilisha Hati ya Kiapo cha Kubadili Jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi.

Mkurugenzi wa Mji,
Halmashauri ya Mji,
S.L.P 28,
UTETE/RUFIJI
Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa “Recruitment Portal”
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKILIWA

DOWNLOAD PDF YA TANGAZO

Mwisho wa Kutuma Maombi ni tarehe 08 Oktoba, 2025

JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?
Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, GROUP NO 2 HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA, GROUP NO 3 HAPA, GROUP NO 4 HAPA


Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *