MATOKEO ya Uchaguzi wa Udahili Kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) Kwa Kozi za Afya na Sayansi Shirikishi 2025/2026 Awamu ya Tatu

MATOKEO ya Uchaguzi wa Udahili Kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) Kwa Kozi za Afya na Sayansi Shirikishi 2025/2026 Awamu ya Tatu
MATOKEO ya Uchaguzi wa Udahili Kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) Kwa Kozi za Afya na Sayansi Shirikishi 2025/2026 Awamu ya Tatu
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) linautaarifu umma kuwa matokeo ya uchaguzi wa awamu ya tatu kwa waombaji wa programu za Afya na Sayansi Shirikishi kwa mwaka wa masomo 2025/2026 yametangazwa rasmi leo tarehe 5 Oktoba, 2025.
Baraza liliratibu udahili wa wanafunzi awamu ya tatu katika kozi mbalimbali za afya na sayansi shirikishi kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) kwa mwaka wa masomo 2025/2026.
Jumla ya waombaji 10,622 walikamilisha maombi yao kwa kuchagua vyuo / programu walizozipenda.
Jumla ya waombaji 9,697 walikuwa na sifa kwenye programu walizoomba na jumla ya waombaji 925 hawakuwa na sifa kwenye programu walizoomba.
Jumla ya waombaji 6,271 wamechaguliwa kujiunga kwenye vyuo vinavyotoa programu mbalimbali za Afya na Sayansi Shirikishi ambapo wanawake ni 3,276(52%) na wanaume 2,995 (48%).
Waombaji 194 walichaguliwa kwenye vyuo vya serikali na waombaji 6,077 katika vyuo visivyo vya serikali.
Aidha, waombaji wenye sifa ambao hawakuchaguliwa kutokana na ushindani katika programu na vyuo walivyoomba, wanashauriwa kuomba kujiunga katika vyuo vyenye nafasi katika dirisha la awamu ya nne na ya mwisho kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja.
Waombaji wote wanaweza kuangalia matokeo ya uchaguzi kupitia tovuti ya Baraza (www.nactvet.go.tz) kwa kubonyeza CAS Selection 2025 kwaajili ya kupata taarifa zaidi.
Baraza linautaarifu umma kuwa dirisha la awamu ya nne na la mwisho limefunguliwa rasmi leo tarehe 5 hadi 15 Oktoba, 2025 na matokeo ya uchaguzi yatatolewa tarehe 21 Oktoba, 2025.
Aidha, kwa anayehitaji kubadilisha programu au chuo, dirisha la uhamisho liko wazi kuanzia tarehe 5 hadi 15 Oktoba, 2025, hivyo atumie dirisha hili kukamilisha maombi hayo kupitia tovuti ya Baraza kwa kubonyeza kwenye akaunti yake aliyotumia kuomba na kuchaguliwa.
JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
