RATIBA ya Mtihani wa Upimaji wa Darasa la Pili 2025

RATIBA ya Mtihani wa Upimaji wa Darasa la Pili 2025
RATIBA ya Mtihani wa Upimaji wa Darasa la Pili 2025
Ratiba ya Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Pili ngazi ya Shule 2025, STNA 2025 Exam Timetable.
Hii hapa Ratiba ya Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Pili Ngazi ya Shule (Standard two School based National Assessment Timetable) Novemba, 2025
DOWNLOAD RATIBA HAPA
MAELEKEZO KWA WALIMU WAKUU
- Hakikisha kuwa unayo Ratiba ya Upimaji wa mwaka 2025 iliyoandaliwa na Baraza la Mitihani la Tanzania.
- Hakikisha kwamba wanafunzi wote waliosajiliwa wanafanya Upimaji wa Stadi ya Kusoma, Kuandika/Writing: Basic English Language Skills na Kuhesabu/Arithmetic Skills.
- Hakikisha kila stadi inafanyika katika tarehe na muda uliooneshwa kwenye ratiba ya Upimaji.
- Ikiwa Shule imesajili wanafunzi zaidi ya 300 ifanye Upimaji wa Stadi ya Kusoma kwa siku mbili tarehe 19.11.2025 na tarehe 20.11.2025.
- Usimamizi wa Upimaji wa Darasa la Pili ufanyike kwa kuzingatia Mwongozo wa Upimaji wa Kitaifa wa Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu Darasa la Pili Ngazi ya Shule unaopatikana kwenye tovuti ya Baraza la Mitihani la Tanzania www.necta.go.tz.
Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
