MAGAZETI ya Leo Jumatatu 10 November 2025

MAGAZETI ya Leo Jumatatu 10 November 2025
MAGAZETI ya Leo Jumatatu 10 November 2025
Wanafunzi wa kidato cha pili takribani 898, 755 wanatarajia kufanya mtihani wa upimaji wa kitaifa (FTNA) Leo Novemba 10, 2025, hadi Novemba 20,2025 katika shule za sekondari 6,238 Tanzania Bara.
Kati ya wanafunzi hao waliosajiliwa kufanya mtihani huo 889,266 ni wanafunzi wa shule ambapo wavulana ni 396,383 sawa na asilimia 44.57 na wasichana ni 492,883 sawa na asilimia 54.43.
Kwa upande wa wanafunzi wa Kujitegemea 9,489 waliosajiliwa, kati yao wavulana ni 4,454 sawa na asilimia 46.94 na wasichana ni 5,035 sawa na asilimia 53.06.
Pia wanafunzi 4,390 wenye mahitaji maalumu wamesajiliwa kati yao, wenye uoni hafifu ni 1,674, wasioona ni 144, uziwi 999, ulemavu wa viungo 1,374 na wenye ulemavu wa akili ni 199.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Profesa Said Mohammed, wanafunzi 2,267 watafanya upimaji wa masomo ya amali kwa mara ya kwanza kwa kuzingatia Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 na Mtaala ulioboreshwa, na wanafunzi 886,999 watafanya mtihani kwa kutumia mtaala wa zamani.
JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
