MAGAZETI ya Leo Ijumaa 28 November 2025

MAGAZETI ya Leo Ijumaa 28 November 2025
MAGAZETI ya Leo Ijumaa 28 November 2025
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), James Kaji amesema kuwa kwa wale wananchi wenye vitambulisho vya NIDA ambavyo vinafutika maandishi sasa wanaweza kuvirudisha na kupewa vitambulisho vipya bure.
Kaji ameyasema hayo Novemba 27, 2025 ambapo amesisitiza kuwa wale wote wanaopitia changamoto hiyo wafike na vitambulisho vyao vinavyofutika maandishi katika Ofisi za Wilaya na kisha watapewa vitambulisho vipya bure huku akisisitiza kuwa wale ambao wameviharibu kwa bahati mbaya au makusudi hawatokuwa kwenye kundi la kubadilishiwa bure bali watatakiwa kulipia gharama za kutengenezewa vitambulisho vipya.
“hivyo sasa tumekuja na suluhu ya vitambulisho vinavyofutika maandishi kama unacho unatakiwa ukirudishe katika Ofisi ya wilaya unaandika jina na unasaini na utapata kitambulisho kipya bila malipo sasa kuna wale ambao wameviharibu mfano mtu alikalia kikavunjika huyo itabidi alipie gharama ya shilingi 20,000 na pia vitambulisho vya kwanza vilivyokuwa na ukomo wa muda tumeondoa ukomo wa vitambulisho lakini kama unaona ile tarehe ya ukomo inakukera njoo lipia alafu tukubadilishie kitambulisho.”
JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
