JINSI ya Kupata Namba ya NIDA Kwenye Simu yako

JINSI ya Kupata Namba ya NIDA Kwenye Simu yako
JINSI ya Kupata Namba ya NIDA Kwenye Simu yako
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inawataarifu wananchi wote kuwa kwa sasa wanaweza kujua Namba yao ya Utambulisho wa Taifa (NIN) kwa urahisi kupitia ujumbe mfupi wa simu (SMS).
Hatua za Kufuata ili Kupata Namba ya NIDA
- Fungua sehemu ya kutuma ujumbe (SMS) kwenye simu yako.
- Andika ujumbe kwa mpangilio ufuatao:
Jina la Kwanza la Mwombaji weka* Jina la Mwisho la Mwombaji weka* Tarehe ya Kuzaliwa (Siku/Mwezi/Mwaka) weka* Jina la Kwanza la Mama weka* Jina la Mwisho la Mama weka
Tuma ujumbe huo kwenda namba 15274.
Huu hapa ni Mfano wa Ujumbe:
MUSA*JUMA*02031987*MARIAM*ALI
Baada ya kutuma ujumbe, utapokea majibu yatakayokuonyesha Namba yako ya Utambulisho wa Taifa (NIN).
Aidha Huduma hii ni BURE.
Zingatia: taarifa unazojaza ni zile zile ulizojaza kwenye Fomu ya NIDA Wakati wa Kujiandikisha, na Spelling zifanane kama ulivyojaza mwanzo unajiandikisha.
Kwa maelezo zaidi, wasiliana na NIDA kupitia:
Tovuti: www.nida.go.tz
Barua pepe: info@nida.go.tz
Mitandao ya kijamii: @nidatzania
JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
