NAFASI Za Kazi Mbeya District Council

Filed in Ajira by on 08.01.2026 0 Comments
Share This Post
NAFASI Za Kazi Mbeya District Council

NAFASI Za Kazi Mbeya District Council

NAFASI Za Kazi Mbeya District Council

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya anapenda kuwatangazia Watanzania Wote kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya imekusudia kuajiri Watumishi wa Mkataba wa kazi ya Muda ya Afisa Muuguzi Msaidizi /Tabibu Daraja la Il aliyesomea mafunzo ya Mwaka mmoja (1) ya (Anaesthesia) ambao watafanya kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya – Kituo cha Afya Ikukwa.

✅AFISA MUUGUZI MSAIDIZI /TABIBU DARAJA LA II NAFASI (02)

SIFA ZA KUAJIRIWA

  • Awe amehitimu kidato cha Nne (IV) au cha sita (VI) na kufaulu. ii. Awe na Leseni ya Uuguzi au Utabibu iliyo hai.
  • Awe amehudhuria mafunzo Usingizi (Anaesthesia) ya mwaka mmoja kutoka katika chuo kinachotambuliwa na serikali
  • Mwombaji awe na cheti cha Diploma ya Uuguzi au Utabibu kutoka katika vyuo vinavyotambulika na serikali.

KAZI ZA KUFANYA

  • Kumwandaa Mgonjwa kabla ya Upasuaji.
  • Kuchunguza Afya yake (Mapigo ya Moyo, shinikizo la Damu, Historia ya Magonjwa).
  • Kutoa Dawa ya Usingizi au kupunguza maumivu.
  • Kufuatilia mgonjwa wakati wa Upasuaji.
  • Kumsaidia Mgonjwa baada ya Upasuaji
    vi. Kufanya kazi nyingine utakazopangiwa na msimamizi wako

MALIPO YA AJIRA KWA NAFASI YA ANAESTHESIA Mshahara kwa mwezi ni TGHS B = Tsh. 865,000/=

MASHARTI YA JUMLA

  • Mwombaji awe Raia wa Tanzania na awe tayari kufanya kazi sehemu yoyote kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
  • Mwombaji awe na umri usiozidi miaka 45 na awe hajawahi kupatikana na kosa la jinai au kufungwa jela.
  • Maombi yote waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V).
  • Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya taaluma, vyeti vya elimu (IV au VI), cheti cha kuzaliwa na picha mbili za rangi za hivi karibuni (Passport size) na iandikwe jina nyuma.
  • Testmonials”,”Provisional Results”,”Statement of results”, hati ya matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU na NECTA).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa UMMA hawataruhusiwa kuomba isipokuwa kama wanakibali cha katibu Mkuu kiongozi.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
  • Awe na Kitambulisho au namba ya Utambulisho wa Uraia kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)
  • Maombi yaandikwe kwa mkono na mwombaji mwenyewe na yawasilishwe Masjala ya wazi ofisi Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.

Barua zote ziandikwe kwa anwani ifuatayo:-
MKURUGENZI MTENDAJI (W)
HALMASHAURI YA WILAYA YA MBEYA,
S.L.P 599,
MBEYA.

Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 16.01.2026 saa 9.30 Alasiri.

JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?
Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, GROUP NO 2 HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA, GROUP NO 3 HAPA, GROUP NO 4 HAPA


Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *