KUITWA Kwenye Usaili Air Tanzania 2026

KUITWA Kwenye Usaili Air Tanzania 2026
KUITWA Kwenye Usaili Air Tanzania 2026
Kampuni ya Ndege Tanzania inapenda kuwataarifu wote walioomba kazi katika kada mbalimbali kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 31 Januari, 2026 hadi tarehe 6 Februari, 2026.
Wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
- Usaili wa mchujo utafanyika tarehe 31 Januari, 2026 na usaili wa mahojiano utafanyika kuanzia tarehe 3 Februari hadi 6 Februari 2026.
- Muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwenye tangazo hili.
- Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi.
- Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkaazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Taifa, Hati
ya Kusafiria au Leseni ya udereva. - Wasailiwa wanatakiwa kufika na vyeti vyao halisi, kuanzia cheti cha Kuzaliwa, Kidato cha IV, VI, Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na
kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji. - Wasailiwa watakaowasilisha “Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo za Kidato cha IV na VI (Form IV and Form VI result slips)
HAZITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI. - Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
- Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
- Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo.
- Wasailiwa wenye tofauti ya majina katika vyeti vya elimu, taaluma na cheti cha kuzaliwa wahakikishe wanakuwa na kiapo cha kubadilisha majina kilichosajiliwa
(DEED POLL). - asailiwa waliozaliwa nje ya Tanzania wahakikishe wanawasilisha uthibitisho wa uraia kutoka Ofisi za Uhamiaji.
JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?DONWLOAD PDF YA MAJINA HAPA
Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
