NAFASI Za Kazi ZAQ Group Ltd

NAFASI Za Kazi ZAQ Group Ltd
NAFASI Za Kazi ZAQ Group Ltd
Kampuni ya ZAQ GROUP LTD yenye makao yake makuu Dar es Salaam inatangaza nafasi za kazi kwaajili ya kiwanda chake cha ushonaji kinachofahamika kwa jina la biashara Streetcode.
✅NAFASI: Mafundi wa Kushona (4)
MAJUKUMU YA KAZI:
- Kushona bidhaa kwa kutumia mashine za viwandani.
- Kuhakikisha ubora wa bidhaa kulingana na viwango vya kampuni.
- Kufanya kazi kwa kufuata vipimo na michoro (patterns).
- Kushirikiana na timu kufikia malengo ya uzalishaji
SIFA ZA WAOMBAJI:
- Awe na umri kati ya miaka 18 – 35.
- Awe na afya njema na anaweza kufanya kazi kwa ufanisi.
- Awe anajua kusoma na kuandika.
- Awe na nidhamu, uaminifu na kujituma kazini.
- Awe tayari kufanya kazi kwa shift yoyote (mchana au usiku).
- Awe na uzoefu wa kazi ya kushona angalau miaka miwili (2) katika kiwanda au warsha ya
ushonaji. - Awe na uwezo wa kutumia mashine za kushonea za viwandani (industrial sewing machine).
- Awe na uelewa wa vipimo, ukataji na ushonaji.
- Awe na uwezo wa kufanya kazi kwa kasi bila kupunguza ubora.
- Awe tayari kujifunza mbinu mpya na teknolojia za ushonaji.
- Awe na mtazamo chanya, maono ya kukua kitaaluma, na nia ya kukua pamoja na kampuni.
- Awe na uwezo wa kudumisha ubora wa kazi (quality control) na kufanya marekebisho inapohitajika
JINSI YA KUTUMA MAOMBI:
Waombaji wote wenye sifa wanatakiwa kuwasilisha maombi yao kwa maandishi pamoja na wasifu binafsi (CV) kupitia ofisi za ZAQ GROUP LTD.
Email: Hr@zaq.co.tz
WhatsApp: https://wa.link/89fcuj
Mwisho wa kupokea maombi: 6 /2/ 2026.
Ni waombaji waliokidhi vigezo tu watakaowasiliana nao.
JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
