MATOKEO ya Usaili wa Mchujo Air Tanzania 2026

MATOKEO ya Usaili wa Mchujo Air Tanzania 2026
MATOKEO ya Usaili wa Mchujo Air Tanzania 2026
MATOKEO YA USAILI WA MCHUJO ULIOFANYIKA TAREHE 31 JANUARI, 2026 KATIKA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (UDSM) NA CHUO KISHIRIKI CHA ELIMU DAR ES SALAAM (DUCE)
Kampuni ya Ndege Tanzania inapenda kuwataarifu wasailiwa wote waliofanya usaili wa mchujo tarehe 31 Januari, 2026 katika kada mbalimbali kuwa matokeo ya usaili yametoka na kwamba usaili wa vitendo na Mahojiano utafanyika kuanzia tarehe 3 Februari, 2026 hadi 6 Februari, 2026 Ofisi ya Kampuni ya Ndege Tanzania Makao Makuu (ATC House) – Posta, Dar es Salaam Tanzania kuanzia saa 2:00 asubuhi.
Wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo hapa chini.
- Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi.
- Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkaazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Taifa, Hati ya Kusafiria, Leseni ya udereva au Barua ya Utambulisho kutoka kwenye Ofisi ya Serikali ya Mtaa unaotoka yenye mhuri juu ya picha yako.
- Wasailiwa wanatakiwa kufika na vyeti vyao halisi, kuanzia cheti cha Kuzaliwa, Kidato cha IV, VI, Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na
kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji. - Wasailiwa walioomba nafasi za Afisa Mauzo na Masoko (Sales and Marketing Officers wanapaswa kuwa na cheti halisi cha usafiri wa anga (Aviation
Certificate). - Wasailiwa watakaowasilisha “Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, “Transcript”, hati za matokeo za Kidato cha IV na VI (Form IV and
Form VI result slips) HAZITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI. - Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
- Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
- Wasailiwa wenye tofauti ya majina katika vyeti vya elimu, taaluma na cheti cha kuzaliwa wahakikishe wanakuwa na kiapo cha kubadilisha majina kilichosajiliwa (DEED POLL).
- Wasailiwa waliozaliwa nje ya Tanzania wahakikishe wanawasilisha uthibitisho wa uraia kutoka Ofisi za Uhamiaji.
- Usaili wa Kada ya Afisa Mauzo na Masoko Daraja la I (Sales and Marketing Officer I- Sales Executive) na Afisa Mauzo na Masoko Daraja la I- (Sales and Marketing Officer I Digital Marketing) hazikuwa na usaili wa mchujo, hivyo usaili wake wa mahojiano utafanyika tarehe 4 na 6 Februari, 2026.
DOWNLOAD PDF HAPA
JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
