NAFASI 31 Za Mhandisi Vifaa Tiba Daraja la II MDAs & LGAs

Filed in Ajira by on 13.02.2026 0 Comments
Share This Post
NAFASI 31 Za Mhandisi Vifaa Tiba Daraja la II MDAs & LGAs

NAFASI 31 Za Mhandisi Vifaa Tiba Daraja la II MDAs & LGAs

NAFASI 31 Za Mhandisi Vifaa Tiba Daraja la II MDAs & LGAs

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya and MDAs & LGAs anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 31 kama ilivyoainishwa katika tangazo hili hapa chini

✅MHANDISI VIFAA TIBA DARAJA LA II (BIOMEDICAL ENGINEER II) – Nafasi 31

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kufanya kazi za matengenezo ya vifaa tiba ngazi ya Wilaya (Electronical Equipments).
  • Kutunza kumbukumbu za kazi za ufundi na matengenezo ya vifaa tiba.
  • Kufanya matengenezo ya kinga ya vifaa tiba.
  • Kuagiza vipuli vya vifaa tiba.
  • Kuandaa bajeti ya huduma za matengenezo ya vifaa tiba ngazi ya wilaya.
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na
    elimu, uzoefu na ujuzi wake.

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa waliohitimu wenye Shahada ya Sayansi ya Uhandisi (Vifaa Tiba) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Bodi ya Wahandisi Tanzania.

NGAZI YA MSHAHARA: TGHS D

MASHARTI YA JUMLA

  • Waombaji wote lazima wawe raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wasizidi umri wa miaka 45.
  • Hata hivyo, kwa nafasi za ndani ya Taasisi za Kijeshi: Waombaji wa nafasi zisizo za shahada wasizidi umri wa miaka 25.
  • Waombaji wa nafasi za shahada wasizidi umri wa miaka 30.
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
  • Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
    Mwanasheria/Wakili.
  • Waombaji kazi ambao ni waajiriwa katika Utumishi wa Umma,WASIOMBE na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyopo katika waraka namba CAC45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya
    kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika:-
    Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
  • Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
  • “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTVET). Kwa waombaji wa
    kada zinazohitaji ‘GPA’ waliosoma nje ya Tanzania waambatishe cheti cha ukokotozi wa ‘GPA’ kutoka TCU.
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320,
Mtaa wa Mahakama, Tambukareli,
DODOMA.

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo;https://portal.ajira.go.tz/. (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

DONWLOAD PDF HAPA

Mwisho wa kutuma Maombi ni tarehe 27 February, 2026.

JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?
Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, GROUP NO 2 HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA, GROUP NO 3 HAPA, GROUP NO 4 HAPA


Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *