NAFASI 65 Za Daktari Wa Upasuaji wa Kinywa na Meno Daraja la II MDAs & LGAs

NAFASI 65 Za Daktari Wa Upasuaji wa Kinywa na Meno Daraja la II MDAs & LGAs
NAFASI 65 Za Daktari Wa Upasuaji wa Kinywa na Meno Daraja la II MDAs & LGAs
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya and MDAs & LGAs anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 65 kama ilivyoainishwa katika tangazo hili hapa chini
✅DAKTARI WA UPASUAJI WA KINYWA NA MENO II (DENTAL SURGEON GRADE II) – Nafasi 65
MAJUKUMU YA KAZI.
- Kufanya kazi zote za matibabu hospitalini zinazohusiana na magonjwa ya kinywa na meno.
- Kutoa na kusimamia elimu ya afya ya kinywa na meno.
- Kuboresha afya ya kinywa na meno katika eneo lake la kazi na jamii.
- Kuziba/kukarabati meno, upasuaji, utengenezaji wa meno, kurekebisha mataya (orthodontics).
- Kusimamia wafanyakazi walio chini yake.
- Kuchunguza, kufuatilia na kuzuia milipuko ya magonjwa.
- Kufundisha wanafunzi katika vyuo vya afya vilivyopo eneo lake la kazi.
- Kubuni na kuendesha utafiti na kusambaza matokeo.
- Kubuni na kutayarisha mikakati ya kuinua ubora wa huduma ya fani yake.
- Kuandaa mipango na makisio ya bajeti ya huduma za afya ya kinywa na meno.
- Kushiriki, kuhakiki na kuboresha huduma za afya.
- Kutoa huduma za outreach katika wilaya/mkoa wake.
- Kutunza takwimu na kuzitumia kama inavyoelekezwa katika misingi ya MTUHA.
- Kupanga na kutathimini huduma za afya ya kinywa na meno katika eneo la kazi.
- Kufanya utafiti katika maeneo mbali mbali ya afya ya kinywa na meno.
- Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na
elimu, uzoefu na ujuzi wake.
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Stashahada ya Tabibu wa Meno (Diploma in Clinical Dentistry) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali, pia awe amesajiliwa na Baraza la Madaktari.
NGAZI YA MSHAHARA: TGHS B
MAJUKUMU YA KAZI
- Kufanya kazi zote za matibabu hospitalini zinazohusiana na magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa ya watoto, magonjwa ya akina mama na upasuaji wa
kawaida na wa dharura. - Kutoa na kusimamia elimu ya afya pamoja na kuboresha afya ya jamii katika Wilaya na Mikoa au eneo lake la kazi.
- Kuchunguza, kufuatilia na kuzuia milipuko ya magonjwa.
- Kutunza takwimu na kuzitumia kama inavyoelekezwa katika misingi ya MTUHA.
- Kupanga na kutathimini huduma za afya katika eneo lake la kazi.
- Kufundisha wanafunzi na watumishi waliopo kwenye eneo la kazi.
- Kusimamia na kuelekeza wafanyakazi walio chini yake.
- Kubuni na kuendesha utafiti na kusambaza matokeo.
- Kubuni na kutayarisha mikakati ya kuinua ubora wa huduma ya fani yake.
- Kuandaa mipango na makisio ya bajeti ya huduma za afya.
- Kushiriki, kuhakiki na kuboresha huduma za afya (medical audit and quality improvement).
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada ya Udaktari kutoka Vyuo Vikuu/Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali waliomaliza “Internship” na kupata usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).
NGAZI YA MSHAHARA: TGHS E
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote lazima wawe raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wasizidi umri wa miaka 45.
- Hata hivyo, kwa nafasi za ndani ya Taasisi za Kijeshi: Waombaji wa nafasi zisizo za shahada wasizidi umri wa miaka 25.
- Waombaji wa nafasi za shahada wasizidi umri wa miaka 30.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
- Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili. - Waombaji kazi ambao ni waajiriwa katika Utumishi wa Umma,WASIOMBE na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyopo katika waraka namba CAC45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya
kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika:-
Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates. - Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTVET). Kwa waombaji wa
kada zinazohitaji ‘GPA’ waliosoma nje ya Tanzania waambatishe cheti cha ukokotozi wa ‘GPA’ kutoka TCU. - Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320,
Mtaa wa Mahakama, Tambukareli,
DODOMA.
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo;https://portal.ajira.go.tz/. (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
DONWLOAD PDF HAPA
Mwisho wa kutuma Maombi ni tarehe 27 February, 2026.
JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, GROUP NO 2 HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA, GROUP NO 3 HAPA, GROUP NO 4 HAPA
Tags: NAFASI 65 Za Daktari Wa Upasuaji wa Kinywa na Meno Daraja la II MDAs & LGAs
