MASHABIKI Waiponza Simba SC

MASHABIKI Waiponza Simba SC
MASHABIKI Waiponza Simba SC
Klabu ya Simba imetozwa faini ya Tsh. Milioni kumi kwa kosa la Mashabiki wake kuwarushia chupa za maji waamuzi wa mchezo wa mchezo wao wa sare ya 1-1 dhidi ya Pamba Jiji FC wakati wakitoka katika uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, tukio ambalo limetokea kwa mara ya pili kwa kipindi cha miezi miwili.
Uamuzi huo umetolewa leo Machi 27, 2026 na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Machi 26, 2026 kwa mujibu wa Kanuni ya 47:1 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Klabu na mazingatio ya kosa la kujirudia.
Itakumbukwa mnamo Februari 25, 2026 mashabiki wa klabu hiyo pia walimrushia chupa za maji mchezaji wa klabu ya Dodoma Jiji, William Edgar wakati mchezo baina ya timu hizo ukiendelea kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
