MAGAZETI ya Leo Ijumaa 03 April 2026

MAGAZETI ya Leo Ijumaa 03 April 2026
MAGAZETI ya Leo Ijumaa 03 April 2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi, uhamisho, utenguzi na kumpangia kituo Balozi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi, uhamisho, utenguzi na kupangiwa kituo Balozi ni kama ifuatavyo:-.
Mhe. Prof. Palamagamba John Aidan Kabudi (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Kabla ya uteuzi huu, Mhe. Kabudi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Ikulu (Kazi Maalum);
Mhe. Reuben Nhamanilo Kwagilwa (Mb.) amehamishwa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwenda kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).
Mhe. Dkt. Festo John Dugange (Mb.) amehamishwa kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais kwenda kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Masuala ya Elimu.
Balozi Ali Jabir Mwadini ameteuliwa kuwa Katibu wa Rais.
Dkt. Eveline Wilbard Munisi ameteuliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Bi. Angela Kizigha ameteuliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Balozi Said Othman Yakub amepangiwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ufaransa, na
Uteuzi wa Dkt. James Andilile Mwainyekule, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) umetenguliwa na atapangiwa majukumu mengine.
Aidha, uapisho wa Waziri na Naibu Mawaziri utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.
