SHERIA Mpya Kombe la Dunia 2026

Filed in Michezo by on 01.04.2026 0 Comments
Share This Post
SHERIA Mpya Kombe la Dunia 2026

SHERIA Mpya Kombe la Dunia 2026

SHERIA Mpya Kombe la Dunia 2026

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Dunia (FIFA) limetangaza mabadiliko matano yatakayotumika kwenye Kombe la Dunia 2026 kwa lengo la kupunguza upotevu wa muda na kuongeza kasi ya mchezo.

Mchezaji anayefanyiwa mabadiliko atapaswa kutoka uwanjani ndani ya sekunde 10. Akichelewa, mchezaji wa kuingia atasubiri dakika moja kabla ya kuruhusiwa kuingia.

Pia, mipira ya kurusha pembeni na golikiki italazimika kuanzishwa ndani ya sekunde tano, vinginevyo timu itapoteza umiliki wa mpira.

Kwa upande wa matibabu, mchezaji anayehudumiwa uwanjani atalazimika kutoka nje kwa dakika moja kabla ya kurejea, isipokuwa kama ameumia kutokana na faulo iliyostahili kadi.

Aidha, VAR sasa itaruhusiwa kupitia kadi ya pili ya njano inayosababisha mchezaji kutolewa, pamoja na kona zilizotolewa kimakosa.

FIFA pia imesisitiza kuwa ni nahodha pekee atakayekuwa na ruhusa ya kumfuata mwamuzi, huku wachezaji wengine wakikabiliwa na kadi ya njano iwapo watamzingira.

Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *