NAFASI Za Kazi Rungwe District Council

Filed in Ajira by on 19.09.2025 0 Comments
Share This Post
NAFASI Za Kazi Rungwe District Council

NAFASI Za Kazi Rungwe District Council

NAFASI Za Kazi Rungwe District Council

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri (W) ya Rungwe anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi za kazi kumi na moja (11) katika Halmashauri hii baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mchanganuo ufuatao:-

✅DEREVA II – NAFASI 4

MAJUKUMU YA KAZI DEREVA II

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
  • Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kazi.
  • Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
  • Kutunza na kuandika daftari la safari “ log book’’ kwa safari zote.
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
  • Kufanya usafi wa gari na
  • Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu kidato cha nne (IV) na kupata cheti cha mtihani wa kidato cha Nne (Form IV) na leseni ya daraja la ‘C’ au ‘E’ ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali. awe amehudhuria
mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingazia Ngazi ya Mishahara ya Serikali TGS –B

✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI II – NAFASI 3

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri.
  • Kupokea wageni na kuwasikiliza shida zao, na kuwaelekeza sehemu
    wanapoweza kusaidiwa.
  • Kutunza taarifa na kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine.
  • Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi.
  • Kupokea majalada na kusambaza kwa maofisa walio katika Idara/Kitengo/ Sehemu husika.
  • Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika.
  • Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali na
  • Kuandaa orodha ya mahitaji ya ofisi.

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amahitimu kidato cha nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) na kupata cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI). Awe na Stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA level 6 ya uhazili kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali. Aidha, awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa
dakika moja na Awe amepata mafunzo ya programu za kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, Powerpoint, Internet, Email na Publisher.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingazia Ngazi ya Mishahara ya Serikali TGS –C

✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II- NAFASI 4

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye rejista (incoming correspondence register).
  • Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasisi kwenye rejista (outgoing correspondence register).
  • Kusambaza majalada kwa watendaji (Action Officers).
  • Kupokea majalada yanayorudi masjala toka kwa watendaji (Action Officers).
  • Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/majalada yanayohitajika na watendaji (Action Officers).
  • Kurudisha majalada kwenye shubaka/kabati la majalada (ranks/filling cabinets) au
    mahali pengine yanapohifadhiwa.
  • Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya taasisi ( File tracking);

SIFA ZA MWOMBAJI:
Awe amehitimu kidato cha nne (IV) au kidato cha sita (IV) na kupata cheti cha mtihani wa Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI). Awe amehitimu mafunzo ya Stashahada/Diploma NTA level 6 katika fani Masjala kutoka vyuo vinavotambuliwa na serikali, pia awe na ujuzi wa kompyuta.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingazia Ngazi ya Mishahara ya Serikali TGS –C

MASHARTI YA JUMLA KWA MUOMBAJI

  • Waombaji wote wawe raia wa Tanzania na wenye umri kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini.
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwaajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
  • Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detail Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya
    Barua pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na Vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
    Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Proffessional Certificate from Respective Boards)
  • Waombaji watakaowasilisha “Testmonial” “Provisioinal Result”,”Statement of result”, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Wapombaji waliosoma nje Nchi wahakikishe vyeti vyao vinahakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA NA NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji wa kazi wa kada ya Dereva II wenye leseni Daraja ‘E’ au ‘C’ wanapaswa KUAMBATISHA vyeti vya mafunzo ya Udereva vilivyowapatia sifa ya kupata
    madaraja husika.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
    Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Waombaji watakaowasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.
  • Wasailiwa ambao majina yao yanatofautiana katika nyaraka zao wanapaswa kuwasilisha Hati ya Kiapo cha kubadili Jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi.

MUHIMU: Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-
MKURUGENZI MTENDAJI
HALMASHAURI YA WILAYA YA RUNGWE
S. L. P 148
RUNGWE

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anauani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ .

Anuani hii inapatikana pia kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’.

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIKIWA.

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUNGWE 19-09-2025

Mwisho wa kutuma Maombi ni tarehe 01 Oktoba, 2025

Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *