MAGAZETI ya Leo Alhamisi 23 October 2025

MAGAZETI ya Leo Alhamisi 23 October 2025


Nahodha wa Simba SC, Shomari Kapombe ametajwa kwenye orodha ya wachezaji 10 wanaowania tuzo ya Mchezaji Bora wa mwaka 2025 wa Shirikisho la soka Afrika CAF kwa wachezaji wa ndani inayowaniwa pia na mshambuliaji wa Pyramids Fc, Fiston Kalala Mayele.
Wachezaji wengine wanaowania tuzo hiyo ni pamoja na mshambuliaji wa Al Ahli ya Libya, Ismail Belkacemi, kiungo wa Pyramids, lbrahim Blati Touré, aliyekuwa beki wa RS Berkane, Issoufou Dayo ambaye ametimkia Umm Salal Sc ya Qatar na winga Emam Ashour wa Al Ahly.
Wengine ni aliyekuwa winga wa Pyramids, Ibrahim Adel ambaye ametimkia Al Jazeera Fc ya Saudi Arabia, nahodha wa AS FAR Rabat, Mohamed Hrimat, beki wa Pyramids, Mohamed Chibi na mshambuliaji wa RS Berkane, Oussama Lamlioui.
