MAGAZETI ya Leo Jumatano 12 November 2025

MAGAZETI ya Leo Jumatano 12 November 2025
MAGAZETI ya Leo Jumatano 12 November 2025
Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam imepanga kutoa uamuzi wa uhalali wa hati ya kesi ya uhaini inayomkabili mfanyabiashara Jenifer Jovin (26), maarufu Niffer na wenzake 21, Novemba 25, 2025.
Mahakama hiyo imepanga tarehe hiyo kutoa uamuzi huo, Jumanne, Novemba 11, 2025, baada ya kukamilisha usikilizwaji wa pingamizi dhidi ya hati hiyo lililotolewa na jopo la mawakili wao linaloongozwa na Peter Kibatala.
Leo Mahakama hiyo imesikiliza majibu ya Jamhuri pamoja na majibu ya utetezi dhidi ya majibu ya Jamhuri.
Niffer ambaye alikamatwa mapema kabla ya siku ya kupiga kura na wenzake hao waliokamatwa siku ya kupiga kura, Oktoba 29, 2025 katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam, wakihusishwa na maandamano ya kupinga uchaguzi huo.
Walipandishwa kizimbani mahakamani hapo Ijumaa, Oktoba 7, 2025.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo Wakili Kibatala aliieleza Mahakama wateja wao walipokuwa Polisi waliteswa kwa kupigwa kwa lengo la kuwashinikiza kukubali kuandika na au kusaini maelezo yao ya onyo, na licha ya wengine kujeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao lakini hawakuwahi kupatiwa matibabu.
Hivyo aliomba Mahakama ielekeze msimamizi wa gereza ambako watapelekwa mahabusu iwapatie matibabu na taarifa za matibabu yao ziwasilishwe mahakamani kuwa sehemu ya kumbukumbu za kesi hiyo.
Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamuya anayesikiliza kesi hiyo katika hatua hiyo ya uchunguzi wa awali kabla ya kuhamishiwa Mahakama Kuu yenye mamlaka ya kuisikiliza, alikubaliana nayo na akatoa maelekezo hayo.
Pia, Kibatala alipinga hati ya mashtaka akidai ina kasoro kwa kujumuisha makosa mawili yaani kula njama na kosa mama la uhaini, ambayo hayapaswi kuwekwa katika hati moja.
