TANGAZO la Kuahirishwa Kwa Usaili UTUMISHI Machi 2026

TANGAZO la Kuahirishwa Kwa Usaili UTUMISHI Machi 2026
TANGAZO la Kuahirishwa Kwa Usaili UTUMISHI Machi 2026
Kufuatia uwepo wa Sikukuu ya Eid al-fitr inayotarajiwa kuadhimishwa tarehe 21-22 Machi, 2026, tunapenda kuwataarifu waombaji wote walioitwa kwenye usaili uliopangwa kufanyika tarehe 22 Machi, 2026 kuwa usaili huo hautafanyika kama ulivyopangwa.
Aidha, tarehe mpya ya usaili itatangazwa kupitia akaunti zenu za Ajira Portal, pamoja na tovuti rasmi ya Sekretarieti ya Ajira ambayo ni www.ajira.go.tz na mitandao rasmi ya kijamii ya Taasisi.
Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliosababishwa na mabadiliko haya na
tunawashukuru kwa ushirikiano na uelewa wenu.
Tafadhali endeleeni kufuatilia taarifa
rasmi, na hakikisheni mnafika kwa wakati pindi tarehe mpya itakapotangazwa, mkiwa na nyaraka zote muhimu.
Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea www.ajira.go.tz.
