MUONGOZO wa Kupata Barua ya Utambulisho Kupitia NAPA Kwaajili ya Kuomba Mkopo (HESLB) 2025/2026

MUONGOZO wa Kupata Barua ya Utambulisho Kupitia NAPA Kwaajili ya Kuomba Mkopo (HESLB) 2025/2026
MUONGOZO wa Kupata Barua ya Utambulisho Kupitia NAPA Kwaajili ya Kuomba Mkopo (HESLB) 2025/2026, Jinsi ya Kupata NAPA Reference Number kwaajili ya Maombi ya Mkopo wa HESLB 2025/2026.
Kwa mara ya kwanza katika historia ya utoaji wa mikopo ya Elimu ya juu nchini Tanzania, Bodi ya Mikopo (HESLB) imetangaza kuwa kila mwombaji wa mkopo kwa mwaka wa masomo wa 2025/2026 ni lazima awe na NAPA Reference Number.
Kupitia Ukurasa huu tumekuandalia Jinsi ya Kupata NAPA Reference Number kwaajili ya Maombi ya Mkopo 2025/2026.
NPA ni kifupi cha National Physical Addressing – mfumo wa Anuani za Makazi za Kitaifa unaosimamiwa na Serikali kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, na kutekelezwa kwa kushirikiana na TCRA, Posta, na TAMISEMI.
Mfumo huu hutambua rasmi eneo mtu anapoishi kwa kutumia:
- Jina la mtaa/kijiji
- Namba ya nyumba
- Kata, wilaya na mkoa
- Msimbo wa posta (postal code)
- Landmark au ramani ya eneo
Kuanzia 2025/2026, HESLB inalenga kuwa na mfumo madhubuti wa utambuzi wa waombaji wa mikopo. Kupitia NAPA ili bodi hiyo iweze;
- Kujua mahali unapoishi kwa uhalisia
- Kupunguza udanganyifu wa taarifa
- Kuimarisha ufuatiliaji wa mikopo baada ya masomo
- Kurahisisha huduma za barua, wito au arifa za Kiserikali.
Baada ya malekezo hayo hapa chini tumekuwekea hatua Kwa hatua jinsi ya Kupata NAPA Reference Number 2025/2026.
Hatua ya 1:
- Nenda kwenye ofisi ya mtaa, kijiji au kata unakoishi.
- Uliza kama wamefanya zoezi la anuani za makazi.
- Ikiwa tayari, utapewa fomu ya usajili wa anuani.
- Ikiwa bado, waombe wakusaidie kuandikishwa.
Hatua ya 2:
- Katika fomu au kwa maelezo yao, jaza.
- Namba ya nyumba (ikiwa ipo.
- Mtaa/Kijiji, Kata, Wilaya.
- Majina yako kamili kama yalivyo NIDA.
- Landmark ya karibu (kituo cha afya, shule, barabara nk)
Hatua ya 3:
- Sajili au Hakiki NAPA Mtandaoni (Kama unayo)
- Tembelea: https://napa.mawasiliano.go.tz/
- Ingia au jisajili kwa kutumia Namba ya NIDA.
- Hakiki anuani yako au omba upya ikiwa haipo.
- Baada ya usajili, utapata NAPA Reference Number yenye muundo maalum (mfano: DSM-ILL-003-067)
Hatua ya 4:
- Tumia NAPA hiyo Katika Fomu ya Mkopo HESLB.
- Ingia kwenye mfumo wa maombi ya mkopo wa HESLB: https://olas.heslb.go.tz.
- Kwenye sehemu ya Anuani ya Makazi, andika NAPA yako kama inavyoonekana hapa chini.

Jinsi ya Kupata NAPA Reference Number kwaajili ya Maombi ya Mkopo wa HESLB 2025/2026.
- Hakikisha unahifadhi screenshot au uipake fomu yako.
Hakikisha taarifa zako zinafanana na NIDA, TCU, HESLB.
Kwa mwaka huu wa 2025/2026, kupata NAPA Reference Number ni hatua ya msingi kwa kila mwombaji wa mkopo kupitia HESLB.
Kwa mara ya kwanza, serikali inahakikisha kwamba kila mwanafunzi anayeomba mkopo anatambulika rasmi makazi yake.
Tumia mwongozo huu kama msingi wa kujihakikishia mkopo wako hautakataliwa kwa sababu ya kukosa anuani sahihi.
TAZAMA VIDEO HAPA KWA MALEKEZO ZAIDI
Tags: MUONGOZO wa Kupata Barua ya Utambulisho Kupitia NAPA Kwaajili ya Kuomba Mkopo (HESLB) 2025/2026
